Saturday, June 26, 2021

TANZANIA NA PAKISTAN ZA ADHIMISHA SIKU YA URAFIKI


Tanzania na Pakistan zimefanya madhimisho ya siku ya urafiki wa kihistoria uliodumu kwa muda mrefu baina ya Mataifa haya mawili rafiki, yaliyochazwa na hafla fupi iliyofanyika tarehe 25 Juni 2021 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 

Madhimisho haya ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza, yalihudhuriwa na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali katika jamii kama vile, Wafanyabiashara, Wanadiplomasia, Watendaji na Viongozi kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali, Watendaji wa Jumuiya za Kikanda, Wanasiasa na baadhi ya Viongozi Wastaafu wa Serikali. 

Pamoja na masuala mengine maadhimisho haya yanalenga kukuza zaidi mahusinao ya kibiashara baina ya Tanzania na Pakistan kwa kuwakutanisha wafanyabisha wa pande zote mbili ili waweze kubadilishana uzoefu na kujenga urafiki ambao utawazesha kwa pamoja kutumia na kuibua fursa za kibiashara zinazopatika katika nchi hizi mbili (Tanzania na Pakistan).

Akizungumza katika maadhimisho hayo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameeleza kuwa Tanzania itaendelea kuendeleza na kuboresha mahausiano mazuri yaliyodumu kwa muda mrefu na Pakistan. Ameongeza kusema kuwa Serikali ya Tanzania imejipanga kutumia muhusionao haya mazuri kuibua fursa za kibiashara ambazo zitanufaisha Serikali na raia wa pande zote mbili. “Takwimu za hivi karibuni zinaeleza, kuna zaidi ya kampuni 100 kutoka Pakistan ambazo zimewekeza nchini Tanzania. Ni lengo la Serikali ya awamu ya 6 kuhakikisha kunakuwepo na muafaka mzuri wa kisheria na kitaasisi na mazingira kwa wawekezaji hawa kufanya biashara nchini Tanzania bila bugudha.”

Akizungumza katika maadhimisho hayo Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Mhe. Mohammad Saleem amepongeza Serikali ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi Mahiri Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendele kuchukua hatua za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini. “Tunaendelea kushuhudia juhudi na mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya usimamizi mahiri wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha mazingira ya biashara nchini, hakika jitihada hizi zinatoa matumaini na faraja kubwa kwa wawekezaji waliopo nchini na wale ambao wanania ya kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini”. 

Mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Pakistan na Tanzania yamedumu kwa tariban miaka 54 tokea yalipoanzishwa mwaka 1967 ambapo nchi ya Pakistani ilifungua Ofisi zake za Ubalozi hapa nchini Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwasili katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam kushiriki maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akihutubia hadhara iliyojitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akihutubia hadhara iliyojitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akikabithiwa picha yenye maudhui ya utamaduni wa Pakistani na Mhe. Mohammad Saleem (kulia) Balozi wa Pakistani nchini, kwenye maadhimisho ya maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania.

Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Mhe. Mohammad Saleem akihutubia hadhara iliyojitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote akihutubia hadhara iliyojitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Hafla ya maadhimisho ikiendelea.
Hafla ya maadhimisho ikiendelea.
Hafla ya maadhimisho ikiendelea.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.