Tuesday, May 28, 2024

MABALOZI KUPIMWA UTENDAJI KAZI KWA KUTUMIA VIGEZO/VIASHIRIA MAHSUSI (KPIs)



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) ameeleza kuwa Wizara  imeanzisha utaratibu maalum wa kupima utendaji kazi wa Balozi na Konseli Kuu kwa kutumia vigezo/viashiriki wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara Bungeni jijini Dodoma tarehe 28 Mei, 2024.

Mhe. Makamba ameeleza kuwa ili kuhakikisha Wizara inakwenda sambamba na maono na matarajio ya Mheshimiwa Rais katika utekelezaji wa majukumu yake, mnamo mwezi Aprili mwaka huu Wizara ilifanya kikao na Mabalozi wote, Makonseli Wakuu, Wakuu wa Utawala na Fedha katika Balozi zetu zote duniani pamoja na viongozi na Menejimenti ya Wizara mjini Kibaha, Mkoani Pwani.


Kikao hicho kilikuwa na azma kuu ya kujitathmini na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha utendaji wetu na wajumbe wa mkutano huo walipata heshima ya kumsikiliza Mheshimiwa Rais na viongozi wengine Serikalini.


Kufuatia kikao hicho, Wizara imeanzisha utaratibu mpya wa kupima utendaji kazi wa Mabalozi wetu nje ya nchi ili kuhakikisha kuwa uwakilishi wetu kupitia Balozi zetu unaleta mchango unaopimika kwenye malengo ya wizara na nchi kwa ujumla.  
 
Mfumo huu utaanza kutumika kwenye mwaka ujao wa fedha 2024/2024.

MIRADI MIKUBWA YA VITEGA UCHUMI KATIKA BALOZI YAJA - WAZIRI MAKAMBA


 


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeeleza kuwa inaratibu na kusimamia Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika viwanja vya Balozi za Tanzania nje wakati wa uwasilishaji wa makadirio ya bajeti ya Wizara bungeni jijini Dodoma tarehe 28 Mei, 2024.

Ufafanuzi huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) ambapo ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024, Wizara iliidhinishiwa jumla ya shilingi 17,887,608,000 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, shilingi 8,400,000,000 ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo kwenye balozi zetu.

Hadi kufikia mwezi Aprili, 2024 Wizara imepokea na kutumia fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali kiasi cha shilingi 16,762,726,958.61 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, shilingi 4,780,120,117 zimeelekezwa katika ukarabati wa majengo na ununuzi wa samani kwenye balozi sita (6) za Tanzania nje ya nchi ambazo ni Beijing, Geneva, Ottawa, Brussels, Stockholm na Windhoek. Wizara pia inaendelea na ukarabati wa jengo la zamani la ubalozi wa Tanzania Washington D.C.

Vilevile, Wizara inaendelea na mradi wa ukarabati wa majengo manne ya Ubalozi wa Tanzania Pretoria, Afrika ya Kusini. Mradi huu unahusisha jengo la ubalozi; makazi ya balozi; makazi ya mkuu wa utawala; na makazi ya mwambata utawala. 

Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya Dola za Marekani 523,561.43 sawa na shilingi 1,293,950,000. 


Kwa upande wa Ubalozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia, Wizara imesaini mkataba na Kampuni ya ALLURE CONSTRUCTION PLC ya Addis Ababa kwa ajili ya uendelezaji wa viwanja vya Ubalozi kwa gharama ya Shilingi 1,164,856,025 pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT). Mradi huu umeshaanza ujenzi wa uzio na unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka wa fedha 2024/25. 224.

Vilevile, Wizara imeingia Makubaliano ya ubia na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Kitega Uchumi katika Ubalozi wa Tanzania Nairobi. Mradi huo unahusu kuendeleza kiwanja kilichopo katika eneo la Upperhill jijini Nairobi kwa kujenga majengo pacha ya ghorofa ishirini na mbili (22).

Wizara pia kwa kushirikiana na Mfuko huo wa Hifadhi wa NSSF imekamilisha maandalizi ya nyaraka za kisheria kwa mradi wa Ujenzi wa jengo la Kitega Uchumi Kinshasa DRC. Utekelezaji wa mradi huo utahusisha ujenzi wa jengo la ghorofa ishirini na tano (25).

Mradi mwingine ni; pamoja na vitega uchumi katika viwanja vya Serikali vilivyopo katika balozi za Tanzania Kampala, Uganda, Abuja Nigeria na Lusaka Zambia. 

Katika utekelezaji wa miradi hiyo, Wizara inakamilisha taratibu za kupata washauri elekezi, kufanya upembuzi yakinifu, kupima udongo, kufanya marejeo ya michoro ya majengo husika, kupata vibali vya ujenzi kutoka mamlaka za miji hiyo na kuanza ujenzi.

Aidha, Waziri Makamba ameeleza kuwa katika kuweka mpango madhubuti wa kuendeleza viwanja na milki zake zilizopo nje ya nchi, Serikali imeunda Timu ya Wataalam, ikiwa na jukumu la kuishauri Serikali namna bora ya kuendeleza na kusimamia milki hizo nje ya nchi. 

Maandalizi yanaendelea ya kumpata Mshauri Elekezi mwenye uzoefu wa Kimataifa katika Masuala ya Milki atakayeandaa nyaraka mbalimbali za uwekezaji, miongozo pamoja na kuishauri Serikali namna bora ya uendelezaji wa milki hizo kulingana na maeneo ya Balozi husika.


DIPLOMASIA YA UCHUMI YAPEWA MSUKUMO MPYA- Waziri Makamba



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) ameeleza kuwa msisitizo wa Sera ya Mambo ya Nje ni Diplomasia ya Uchumi wakati akiwasilisha makadirio ya Hotuba ya Bajeti ya Wizara tarehe 28 Mei, 2024 bungeni jijini Dodoma.

Katika hotuba hiyo amelifahamisha Bunge kuwa, Wizara imekamilisha rasimu ya awali ya Mkakati wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi itakayotoa mwongozo wa utekelezaji wa majukumu yake.

”Mkakati huo umeainisha maeneo saba ya kipaumbele ambayo Wizara itayatilia mkazo katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi”, Alisema Waziri Makamba.

Maeneo hayo ni pamoja na; kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi, kuvutia watalii kuja Tanzania, kutafuta misaada na mikopo ya masharti nafuu kutoka nje, kutafuta fursa za ajira na masomo kwa Watanzania nje ya nchi, kujenga taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa, kujenga wezo wa kitaasisi wa Wizara, na Wizara na Taasisi nyingine kusimamia vizuri utekelezaji wa Mkakati wa Diplomasia ya Uchumi.

Aidha, kukamilika kwa mkakati huo kutaiwezesha Serikali na wadau wote kutambua majukumu yao katika mnyororo wa hatua za kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa.

Utekelezaji wa diplomasia ya uchumi umeiwezesha nchi kuingia makubaliano mbalimbali yenye tija kwa Taifa. Makubaliano hayo yamewezesha kupata mikopo nafuu na misaada, kuvutia watalii, kupata masoko ya bidhaa zetu, kuvutia wawekezaji na wabia wa aina mbalimbali wa maendeleo yetu.   

Mafanikio mengine yaliyopatikana ni; kupata masoko ya bidhaa na huduma nje ya nchi, kuwezesha uagizaji bidhaa na huduma muhimu kutoka nje ya nchi ili kukidhi mahitaji ya ndani; na kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje.

Wizara imefanikisha jukumu hilo kwa kushirikiana na Wizara za kisekta, Taasisi za Umma na Sekta Binafsi ambapo zimekuwa zikiratibu makongamano mbalimbali ya biashara na uwekezaji yanayofanyika pamoja na ziara za Mheshimiwa Rais nchi za nje. Vilevile, kuratibu ziara za watendaji wa serikali katika nchi na kuzungumzia masuala ya kiuchumi, biashara na uwekezaji kwa wadau mbalimbali wa maendeleo.

DIPLOMASIA YA UCHUMI YAPEWA MSUKUMO MPYA- WAZIRI MAKAMBA


 


TODAY
MIRADI MIKUBWA YA VITEGA UCHUMI KATIKA BALOZI YAJA Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeeleza kuwa inaratibu na kusimamia Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika viwanja vya Balozi za Tanzania nje wakati wa uwasilishaji wa makadirio ya bajeti yake bungeni jijini Dodoma tarehe 28 Mei, 2024. Ufafanuzi huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) ambapo ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024, Wizara iliidhinishiwa jumla ya shilingi 17,887,608,000 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, shilingi 8,400,000,000 ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo kwenye balozi zetu. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2024 Wizara imepokea na kutumia fedha kutoka…
Read more
16:44
16:45
MUUNDO WA WIZARA KUBORESHWA ILI KUAKISI MAHITAJI YA SASA Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amelieleza Bunge kuhusu jitihada mbalimbali zinazofanywa na Wizara hiyo katika kuboresha utendaji wake. Ufafanuzi huo umetolewa wakati wa uwasilishaji wa makadirio ya bajeti ya wizara uliofanyika bungeni jijini Dodoma tarehe 28 Mei, 2024. Aidha, Waziri Makamba ameeleza kuwa katika kufanikisha hilo Wizara iliunda timu ya ndani ya kujitathmini ambayo ripoti yake iliwasilishwa kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadae katika Baraza la Mawaziri. Pia, Wizara inafanya maboresho ya muundo kwa lengo la kuongeza ufanisi wenye tija ili kuendana na mahitaji halisi ya wakati wa sas…
Read more
16:46

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) ameeleza kuwa msisitizo wa Sera ya Mambo ya Nje ni Diplomasia ya Uchumi wakati akiwasilisha makadirio ya Hotuba ya Bajeti ya Wizara Bungeni jijini Dodoma. 
 
Katika hotuba hiyo amelifahamisha Bunge kuwa, Wizara imekamilisha rasimu ya awali ya Mkakati wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi itakayotoa mwongozo wa utekelezaji wa majukumu yake. 
 
"Mkakati huo umeainisha maeneo saba ya kipaumbele ambayo Wizara itayatilia mkazo katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi”, alisema Waziri Makamba. 
 
Maeneo hayo ni pamoja na kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi, kuvutia watalii kuja Tanzania, kutafuta misaada na mikopo ya masharti nafuu kutoka nje, kutafuta fursa za ajira na masomo kwa Watanzania nje ya nchi, kujenga taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa, kujenga wezo wa kitaasisi wa Wizara, na Wizara na Taasisi nyingine kusimamia vizuri utekelezaji wa Mkakati wa Diplomasia ya Uchumi. 
 
Aidha, kukamilika kwa mkakati huo kutaiwezesha Serikali na wadau wote kutambua majukumu yao katika mnyororo wa hatua za kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa. 
 
Utekelezaji wa diplomasia ya uchumi umeiwezesha nchi kuingia makubaliano mbalimbali yenye tija kwa Taifa. Makubaliano hayo yamewezesha kupata mikopo nafuu na misaada, kuvutia watalii, kupata masoko ya bidhaa zetu, kuvutia wawekezaji na wabia wa aina mbalimbali wa maendeleo yetu. Mafanikio mengine yaliyopatikana ni; kupata masoko ya bidhaa na huduma nje ya nchi, kuwezesha uagizaji bidhaa na huduma muhimu kutoka nje ya nchi ili kukidhi mahitaji ya ndani; na kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje. 
 
Wizara imefanikisha jukumu hilo kwa kushirikiana na Wizara za kisekta, Taasisi za Umma na Sekta Binafsi ambapo zimekuwa zikiratibu makongamano mbalimbali ya biashara na uwekezaji yanayofanyika pamoja na ziara za Mheshimiwa Rais nchi za nje. 
 
Vilevile, kuratibu ziara za watendaji wa serikali katika nchi na kuzungumzia masuala ya kiuchumi, biashara na uwekezaji kwa wadau mbalimbali wa maendeleo.



Friday, May 24, 2024

MIAKA 20 YA BARAZA LA AMANI NA USALAMA AFRİKA RAIS MSTAAFU WA NIGERIA MHE. OBASANJO AWASILI NCHINI

Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo akiwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipowasili nchini tarehe 24 Mei 24 kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika.

 

Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaibu Mussa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipowasili nchini tarehe 24 Mei 24 kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika.

Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaibu Mussa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipowasili nchini tarehe 24 Mei 24 kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika

 


 

Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo amewasili nchini leo tarehe 24 Mei 24 kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini  Dar es Salaam Mhe. Obasanjo alilakiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa.

Mhe. Obasanjo ni miongoni mwa Marais Wastaafu na viongozi wengine wa Nchi za Afrika, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa ambao watashiriki maadhimisho hayo yatakayofanyika nchini tarehe 25 Mei,2024.

Maadhimisho ya Miaka 20 ya Baraza hilo yataongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC)

 
Uenyeji wa Tanzania katika maadhimisho hayo unatokana na maamuzi ya Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi Februari 2024 jijini Addis Ababa, Ethiopia ambapo Tanzania ilichaguliwa tena kuhudumu kwenye Baraza hilo kwa muhula mwingine wa miaka miwili hadi mwaka 2026.
 
Baraza la Amani na Usalama ni chombo cha juu cha maamuzi kuhusu masuala ya amani na usalama kwenye Umoja wa Afrika likiwa na jukumu la kuzuia kutokea kwa migogoro, kusuluhisha au kukabiliana nayo pale inapojitokeza.
 
Nchi 15 tu kati ya nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika ndio wajumbe wa Baraza hilo na  wajumbe wa sasa ni; Tanzania, Uganda , Djibout, Cameroon, DRC,  Equatorial Guinea ,Afrika Kusini, Angola, Botswana, Cote d’Ivoire , Gambia, Nigeria,  Sierra Leone,  Misri na Morocco.
 
Kwa mwezi huu wa Mei, Tanzania ni Mwenyekiti wa Baraza hilo na kuwa Mjumbe kwenye Baraza hili ni ishara ya kuheshimika na kuaminika kwa nchi na Katika nafasi ya Uenyekiti Tanzania inajukumu la kusimamia shughuli zote zinazohusu Baraza, ikiwemo kufuatilia kwa karibu hali ya ulinzi na usalama kwenye Bara la Afrika, kutoa miongozo ya kushughulikia na masuala ya kiusalama pale inapobidi na pia kuandaa ratiba na kuongoza vikao vya Baraza.
 
Katika maadhimisho hayo Tanzania kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Baraza iliaandaa shughuli mbalimbali zilizofanyika  kila wiki katika mwezi Mei ambazo zilibeba dhima mahsusi za: Usuluhishi na majadiliano; masuala ya mahitaji ya kibinadamu,amani na usalama; ulinzi kwa Watoto na kusaidia misheni za amani.
 
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya Miaka 20 ya Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika ni; ‘’Miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika ikiwa chombo cha Maamuzi: Miongo miwili ya Afrika ya tuitakayo.
 
Maadhimisho haya, yanatoa fursa kwa Waafrika wote wenye kuitakia mema Afrika kutoa maoni yao ya kuliimarisha Baraza ili liweze kushughulikia changamoto za kiusalama barani Afrika ambapo wageni takriban 120 kutoka nchi mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria maadhimisho hayo
 
Mbali na Mhe. Obasanjo, Rais Rais Mstaafu wa Burundi, Mhe. Domitien Ndayizeye, Rais Mstaafu wa Msumbiji, Mhe. Joachim Chissano na Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pia watahudhuria maadhimisho hayo ambayo yatahitimishwa kwa kutolewa kwa Tamko la Dar es Salaam.

Wednesday, May 22, 2024

WAZIRI MAKAMBA AAGANA NA BALOZI WA ITALIA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba ameagana na Balozi wa Italia nchini ambaye amemaliza muda wake wa utumishi nchini hapa nchini.

Akizungumza katika kikao hicho Waziri Makamba amemtakia kila la heri Balozi Lambardi na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Italia.

“Uliukuta uhusiano wa Tanzania na Italia ukiwa katika hali nzuri lakini kwa nguvu, jitihada na weledi wako umeufanya uhusiano wetu kuwa katika kiwango cha juu kabisa, tunakupongeza na kukushukuru sana,” alisema Waziri Makamba.

Naye Balozi Lambardi ameishukuru Wizara na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano mkubwa iliyompatia wakati wote ambao amekuwa kitekeleza majukumu yake nchini.

“Mhe. Waziri niwashukuru sana Wizara na hasa Idara ya Ulaya na Amerika kwa kushirikiana nami na kufanya utendaji wangu kukamilika bila kukwama, asanteni sana” alisema Balozi Lambardi.

Amesema ana amani kuwa anaondoka nchini huku akiuacha mpango wa Matei ukiwa katika hatua nzuri ya utekelezaji.










 


TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA

 

 

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (PSC-AU) yatakayofanyika tarehe 25 Mei, 2024 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amefafanua kuwa, uenyeji huu umekuja kufuatia maamuzi ya Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi Februari 2024 jijini Addis Ababa, Ethiopia.

 

“Ikumbukwe kuwa, mwezi Machi 2022 Tanzania ilichaguliwa kuhudumu kwenye nafasi ya Mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kwa miaka miwili hadi mwezi Machi 2024 ambapo muda wa kuhudumu ulifikia kikomo. Hivyo Tanzania imechaguliwa tena kuhudumu kwenye Baraza hilo kwa muhula mwingine wa miaka miwili hadi mwaka 2026,” alisema Mhe Waziri.

 

Amesema Baraza la Amani na Usalama ni chombo cha juu cha maamuzi kuhusu masuala ya amani na usalama kwenye Umoja wa Afrika likiwa na jukumu la kuzuia kutokea kwa migogoro, kusuluhisha au kukabiliana nayo pale inapojitokeza.

 

Amesema Nchi 15 tu kati ya nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika ndio wajumbe wa Baraza hilo na kuongeza kuwa  wajumbe wa sasa ni pamoja na; Tanzania, Uganda na Djibout (Ukanda wa Afrika Mashariki); Cameroon, DRC na Equatorial Guinea (Kanda ya Kati); Afrika Kusini, Angola na Botswana (Kanda ya Kusini); Cote d’Ivoire , Gambia, Nigeria, na Sierra Leone (magharibi) na Misri na Morocco (Ukanda wa Kaskazini).

 

‘’Hivyo, Tanzania kuwa Mjumbe kwenye Baraza hili ni ishara ya kuheshimika na kuaminika kwa nchi yetu, ambapo heshima hiyo inaifanya nchi yetu kupewa jukumu jingine kubwa zaidi la kuwa mwenyekiti wa Baraza hilo kwa mwezi Mei. Katika nafasi ya Uenyekiti Tanzania inajukumu la kusimamia shughuli zote zinazohusu Baraza, ikiwemo kufuatilia kwa karibu hali ya ulinzi na usalama kwenye Bara la Afrika, kutoa miongozo ya kushughulikia na masuala ya kiusalama pale inapobidi na pia kuandaa ratiba na kuongoza vikao vya Baraza,’’ alisema Waziri Makamba.

 

Pia Mhe. Makamba ametumia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya ya kuimarisha Diplomasia ya Tanzania katika kutoa kipaumbele kwenye masuala ya ulinzi na usalama barani Afrika na dunia kwa ujumla.

 

Katika maadhimisho hayo Tanzania kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Baraza imeandaa ratiba ya shughuli mbalimbali kwa kuifanya kila wiki katika mwezi Mei kubeba dhima mahsusi ambazo ni: Usuluhishi na majadiliano; masuala ya mahitaji ya kibinadamu,amani na usalama; ulinzi kwa Watoto na kusaidia misheni za amani.

 

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya Miaka 20 ya Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika ni; ‘’Miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika ikiwa chombo cha Maamuzi: Miongo miwili ya Afrika ya Amani na Usalama tunayoitaka  (20 years of the AU PSC as a Standing Decision-Making Organ: The Next Decades of the Peace and Security We Want in Africa)’’

 

Maadhimisho haya, yanatoa fursa kwa Waafrika wote wenye kuitakia mema Afrika kutoa maoni yao ya kuliimarisha Baraza ili liweze kushughulikia changamoto za kiusalama barani Afrika. Hivyo, wageni takriban 120 kutoka nchi mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria.

 

Kadhalika, Miongoni mwa watu mashuhuri watakaoshiriki ni pamoja na; Mhe. Jesca Alupo, Makamu wa Rais Uganda, Mhe. Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Rais Mstaafu wa Nigeria, Mhe. Olesegun Obasanjo, Rais Mstaafu wa Burundi, Mhe. Domitien Ndayizeye, Rais Mstaafu wa Msumbiji, Mhe. Joachim Chissano na Rais wetu Mstaafu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

 

Mhe. Waziri Mkamba ametoa rai kwa watanzania kushiriki kwa wingi katika siku ya tarehe 24 Mei, 2024 ambako kutakuwa na mjadala wa wazi utakaofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na siku ya kilele cha maadhimisho hayo ili kumuunga mkono Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa heshima kubwa aliyopewa na Umoja wa Afrika.

 

Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza yatahitimishwa kwa kutolewa kwa Tamko la Dar es Salaam.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 22 Mei, 2024.

Kutoka kushoto Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Afrika Addis Ababa, Ethiopia Mhe. Balozi Innocent Shiyo pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga.

Mkutano ukiendelea.




 

 

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akisalimiana na Naibu Waziri  wa Mambo ya Nje wa Japan  Mhe. Kiyoto Tsuji walipokutana katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa  Mambo ya Nje wa Japan Mhe. Kiyoto Tsuji walipokutana katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

 

  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan  Mhe. Kiyoto Tsuji (hayupo katika picha) walipokutana katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

 

  

kikao kikiendelea

 

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje  wa Japan Mhe. Kiyoto Tsuji akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba  walipokutana katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

 

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Mhe. Kiyoto Tsuji akizungumza walipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba   katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Mhe. Kiyoto Tsuji akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba  (hayupo pichani) walipokutana katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

 

kikao kikiendelea

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Mhe. Kiyoto Tsuji akizungumza alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba  walipokutana katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Mhe. Kiyoto Tsuji aliyemtembelea  katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Mhe. Kiyoto Tsuji katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

 

Viongozi hao katika mazungumzo yao wamekubaliana kuendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu kwa manufaa ya nchi na wananchi wake.

 

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Waziri Makamba ameishukuru  Serikali ya Japan kwa kuendelea kuwa mdau mzuri wa maendeleo kwa Tanzania ambapo imekuwa ikiipatia Tanzania misaada mbalimbali ambayo imekuwa mchango chanya  kwenye maisha ya Watanzania wengi na hivyo kusaidia jitihada za Serikali kufikia maendeleo makubwa ya kiuchumi na kuhakikisha maisha bora kwa wananchi wake.

 

Ametaja misaada ambayo Tanzania inapokea kama misaada kutoka Serikali ya Japan kuwa ni pamoja na miradi ya ujenzi wa, barabara ya mzunguko ya Dodoma, barabara ya Holili Arusha na Soko la Malindi Zanzibar kuwa ni miongoni mwa maeneo ambayo Tanzania imenufaika nayo kupitia uhusiano na ushirikiano na Japan.

 

“Nitumie nafasi hii kuishukuru Serikali ya Japan kwa kukubali kwake mradi wa Upanuzi wa bandari ya Kigoma ambao utaiunganisha Tanzania na Mashariki mwa nchi ya DRC pamoja na Zambia na Burundi ambazo pia ni watumiaji wa Ziwa Tanganyika,” alisema Mhe. Waziri.

 

Amesema Tanzania imejipanga kuhakikisha inaongeza kiwango cha biashara na uwekezaji kati yake na Japan na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi kwa manufaa ya pande zote mbili.

 

Amesema Tanzania na Japan zimekuwa zinashirikiana kupitia maeneo ya elimu kwa kusaidia kujenga uwezo kwa Watanzania, afya, miundombinu, nishati jadidifu Diplomasia na ushirikiano wa kimataifa.

 

Naye Mhe. Tsuji ameeleza utayari wa Japan kuendelea kushirikiana na Tanzania  kuimarisha uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Japan.

 

Ameipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika masuala ya amani duniani kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa na nchi nyingine na hivyo kutoa mchango mkubwa kwa uwepo wa amani na usalama duniani.

 

Amesema Japan iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuongeza biashara na bara la Afrika na kushirikiana kukuza ushirikiano na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kwa manufaa ya pande zote mbili.