Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akielezea kuhusu hisia za kutengwa kwa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Waziri Membe alikuwa katika mahojiano maalum na Mwandishi Fredy Mwanjala wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.
Waziri Membe akiendelea na mahojiano hayo, wakati Bi. Fauzia Yusuph wa Channel Ten akirekodi tukio hilo.
Jumuiya
ya EAC na talaka rejea
Na TAGIE
DAISY MWAKAWAGO
Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) ameelezea hisia za
sintofahamu kuhusu kutengwa kwa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC), na kuhoji kuwa iwaje nchi yetu itengwe na nini maana ya Jumuiya hiyo?
Aliyasema hayo katika
mahojiano maalum na Mwandishi Fredy Mwanjala wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, yaliyofanyika ofisini kwake
leo, jijini Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalijikita zaidi katika kujua
msimamo wa Tanzania kidiplomasia wakati huu wa sintofahamu ya Jumuiya hiyo
inayoendelea, hususan Tanzania ikionekana kutengwa na nchi za Uganda, Rwanda na
Kenya.
“Huu ni muungano wa
watu wenye woga,” alisema Waziri Membe na kuongeza kuwa Jumuiya hiyo ilishawahi
kuvunjika mnamo mwaka 1977.
“Jumuiya hiyo
ilishawahi kuvunjika na kuungwa tena, na Tanzania hatukuathirika. Tuko tayari kupewa au kutoa talaka, na ikiwezekana
labda kutakuwa na talaka rejea,” alisema Waziri Membe. Jumuiya hiyo ya EAC inazijumuisha nchi za
Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na Tanzania.
“Sisi ndio ‘center of gravity’ na ndio soko kubwa
la bidhaa katika ukanda wa Afrika Mashariki - tuna rasilimali zaidi ya majirani
zetu, tuna utajiri wa ardhi na bandari nne ambazo ni ufunguo wa kutumia bahari
kubwa na kufikia nchi nyingine duniani,” alifafanua Waziri Membe. Bandari hizo ni za Mtwara, Tanga, Dar es
Salaam na bandari ya Bagamoyo ambayo ipo katika ujenzi wa kuifanya iwe bandari
kubwa ya kimataifa barani Afrika.
Waziri Membe alisema
cha kushangaza ni kwamba majirani zetu wanatakiwa kutambua kuwa Tanzania ni
nchi ambayo ni mfano pekee wa kuigwa kwa uzoefu wa muungano. “Sisi ni taifa na sio muungano wa makabila
matatu au manne,” alisema Waziri huyo.
“Hauwezi leo
ukaitaifisha ardhi ya nchi nyingine na kuviacha vizazi vijavyo bila mali,”
alisema Waziri Membe na kuongeza kuwa “kwa vyovyote vile, jumuiya hii ya Afrika
Mashariki lazima iende kwa taratibu.”
Aidha, Waziri Membe
alienda mbali zaidi na kusema kuwa huenda chokochoko ya kutengwa kwetu
inatokana na wivu au gere kwa Tanzania kupeleka majeshi yake huko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jambo alilosema huenda halijawafurahisha baadhi ya watu katika Jumuiya
hiyo.
Vilevile alisema kuwa
kitendo cha Tanzania kukataa ardhi kuwa sehemu ya mali ya Afrika Mashariki
huenda pia imepelekea mchango mkubwa kwenye choko choko hizo.
Waziri Membe
amewaambia Watanzania kuwa “wakae wakijua kwamba akufukuzae hakwambii toka,
utaona tuu mambo yanabadilika.”
Mwisho.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.