Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale (kulia) na Meneja Mkuu wa Kampuni ya SUMITOMO MITSUI, Bw. Ichiro Aok kutoka Japan wakiweka saini Mkataba wa kuanza ujenzi wa barabara ya juu (flyover) katika eneo la TAZARA.
SUMITOMO MITSUI ni kampuni iliyoshinda zabuni ya kujenga barabra hiyo, ambao ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi Novemba 2015 na kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu.
Wengine katika picha waliosimama watatu kutoka kulia ni Waziri wa Ujenzi na Mgombea wa nafasi ya Rais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, kushoto kwake ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida na Mwakilishi Mkazi wa JICA nchini Tanzania. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.