Taarifa zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki na kujeruhiwa huko Saudi Arabia
Mahujaji wengine wanane kutoka Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tokea ajali ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe 24 Septemba 2015 wametambuliwa kuwa, ni miongoni mwa mahujaji waliofariki dunia. Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania walipoteza maisha katika ajali hiyo kufikia ishirini (20). Majina kamili ya mahujaji hao na vikundi vilivyowasafirisha kwenda Makkah katika mabano ni Hamida Llyas Ibrahim (Khidmat Islamiya), Farida Khamis Mahinda (Ahlu Daawa), Archelaus Anatory Rutayulungwa (Khidmat Islamiya) na Said Abdulhabib Ferej (Ahlu Daawa).
Wengine ni Awadh Saleh Magram (Khidmat Islamiya), Salama Rajab Mwamba (Khidmat Islamiya), Nuru Omar Karama (Ahlu Daawa) na Saida Awaadh Ali (Ahlu Daawa).
Serikali ya Saudi Arabia inaendelea kutoa taarifa zaidi za mahujaji waliofariki dunia au kujeruhiwa katika ajali hiyo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu wahanga wa ajali hiyo kadri itakapokuwa inazipokea.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
13 Oktoba, 2015
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.