Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzani katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi,
akichangia majadiliano kuhusu upokonyaji wa silaha na usalama wa kimataifa
mwishoni mwa wiki, ambapo ametoa wito wa jumuiya ya kimataifa
kushirikiana katika kuhakikisha kuwa silaha za maangamizi haziishii
mikononi mwa makundi ya kihalifu.
Na Mwandishi Maalum, New York
TANZANIA imetoa wito Kwa Jumuiya ya Kimataifa
wa kuhakikisha inashirikiana kuhakikisha kwamba silaha za
maangamizi zikiwamo za nyukilia haziiangukii mikono ya
makundi ya kihalifu.
Wito huo umetelewa mwishoni mwa wiki na Mwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako
Manongi,wakati wa Mkutano kuhusu masuala ya uponyaji wa silaha
na usalama wa kimataifa.
Katika mkutakno huo wazungumzaji wengi walieleza
wasiwasi wa kuwapo kwa ushirikiano wa karibu kati ya nchi ambazo
zina silaha za nyukilia na zile ambazo hazina, lakini huku zile ambazo
zinamiliki silaha hizo zikiendelea kuziboresha na kujilimbikizia.
“Ni jambo la kusikitisha, badala ya kuzipungua silaha
hizi na hatimaye kuzitokomeza kabisa, nchi zinazolimiki silaha za
nyukilia zinaendelea na kasi ya kuziboresha , kuzifufua na
kujilimbikiza”. Akasema Balozi Manongi.
Akabainisha kuwa mbaya Zaidi hata zile nchi ambazo hazina
silaha hizo nazo sasa zinatafuta kila maarifa ya kuwa nazo. Jambao
ambalo amesema ni tishio kwa usalama wa mwanadamu.
Amesisitiza kuwa ingawa ni miongo saba imekwisha kupita
lakini madhara ya matukio ya Hiroshima na Nagasaki bado yanaendelea
na yapo hai miongoni mwetu.
Balozi Manongi akaongeza kuwa ni muhimu basi utokomezaji wa
silaha za nyukilia na teknolojia inayoambatana nazo likaendelea
kupewa kipaumbele pamoja na kuwa na mikataba ya kisheria
itakayosimamia jambo hilo.
Akasema kutoka na ongezeko la ulimbikizaji wa silaha
za nyukilia, Jumuia ya kimataifa inawajibu wa kushirikiana kuhakikisha
kwamba silaha hizo na nyingine za maangamizi haziangukii mikononi mwa
makundi ya kigaidi na kihalifu.
Pamoja na ukweli kwamba silaha za nyukili na zingine za
maangamizi bado ni tishio kubwa kwa uhai wa mwanadamu. Balozi Manongi
akasema kwa nchi zinazoendelea tatizo la usaambaji na matumizi holela ya
silaha ndogo na nyepesi zinaendelea kuwa janga kubwa kwa ustawi na
maendeleo ya bara hili na kwingineko.
Akimnukuu Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi
Annan kwamba madhara yatokanayo na matumizi holela ya
silaha ndogo na nyepesi yameendelea kuwa makubwa sana na
madhara yake ni makubwa pengine kuzidi mabomu ya
atomic yaliyoiangamizia Hiroshima na Nagasaki.
Akizungumzia zidi kuhusu matumizi holela ya silaha ndogo na
nyepesi, Mwakilishi huyo wa Tanzania anasema mirindimo
ya risasi na hata matumizi ya silaha kali zikiwamo za
maangamizi, haiwezi au haitamhakikishia
mwananchi maisha yenye hadhi, utu, ustawi na maendeleo.
Akasema kuna uhusiano mkubwa baina ya Amani, usalama na
utekelezaji wa Malengo ya maendeleo endelevu y (Agenda 2030) malengo
yanayojikita katika kumaliza umaskini pasipo kumwacha yoyote nyuma pamoja
na kuilinda sayari dunia.
Akasema itakuwa vigumu kuyatekeleza malengo
mapya ya maendeleo kama kiwango cha gharama za kujilimbikiza silaha
kitaendelea ambapo inakadiriwa kuwa mataifa hasa yale makubwa
yanatumia Zaidi ya dola za kimarekani trillion 1.7 kwa mwaka kwa
matumizi ya silaha.
Akasema matumizi ya kiasi hicho cha fedha
kujilimbikizia silaha katika maghara mbalimbali duniani huku
mamilioni ya watu wakiendelea kuishi katika umaskini uliopindukia, na
maelfu ya watoto wakiathirika kwa utapia mlo na wengine wakipoteza maisha kwa
kukosa chakula na huduma nyingine za msingi ni jambo lisilo kubalika.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.