Rais Kikwete akipiga makofi kuonesha furaha yake kuwa Wizara ya Mambo ya Nje itapata ofisi za kisasa hivi karibuni |
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga akitoa neno la kuwakaribisha wageni waalikwa akiwemo Rais Kikwete katika hafla ya kumuaga. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akitoa utambulisho wa wageni waalikwa wakiwemoWaheshimiwa Mabalozi waliostaafu. |
Balozi Mstaafu akisalimia wajumbe baada ya kutambulishwa |
Watumishi wa Wizara wakiwemo Wakuu wa Idara/Vitengo, Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi wakiwa wameketi kwa ajili ya kushuhudia matukio ya hafla ya kumuaga Rais Kikwete. |
Sehemu ya watumishi wa Wizara waliohudhuria hafla ya kumuaga Rais Kikwete |
Watumishi wa Wizara katika hafla ya kumuaga Rais Kikwete |
Mtumishi wa Wizara akisoma utenzi wa kumsifu na kumpongeza Rais Kikwete namna alivyoongoza Taifa la Tanzania kwa umahiri mkubwa katika kipindi chake cha miaka 10 ambacho kinakamilika Oktoba 2015. |
Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Bernard K.Membe akisoma hotuba yake katika hafla hiyo. Hotuba ya Waziri Membe iligusia mafaniki ambayo Serikali ya awamu ya nne imeyapata katika kipindi cha miaka 10 ikiwa ni pamoja na kuvutia wawekezaji wakubwa, kuongeza uwakilishi nje ya nchi,kujenga ofisi za kibalozi na utatuzi wa migogoro. |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Membe wakionesha Tuzo aliyotunukiwa Rais Kikwte na Wizara ya Mambo ya Nje. |
Picha za juu zinaonesha zawadi mbalimbali ambazo Rais Kikwete amekabidhiwa wakati wa hafla hiyo |
Picha ya pamoja kati ya Mhe. Rais Kikwete, Mhe. Waziri Membe, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje,Wakuu wa Idara/Vitengo na Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi |
Mhasibu Mkuu wa Wizara, Bw. Paul Kabale akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.