========================================
Konseli Mkuu wa Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania uliopo Jeddah, Saudi Arabia, Bw. Suleiman Saleh, Jumanne
Machi 29, 2016, amekaribishwa rasmi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi
Arabia alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi Muhammad A. Tayeb,
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara hiyo.
Balozi Tayeb alimpokea Bw. Saleh Ofisini kwake
Jeddah na kuahidi kutoa ushirikiano unaohitajika katika kuimarisha mahusiano
baina ya Saudi Arabia na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kusainiwa
hivi karibuni Ikulu, Dar-es-Salaam, makubaliano ya mashirikiano baina ya nchi
hizo mbili. Makubaliano hayo ambayo yalisainiwa na Mhe. Adil Jubeir,
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia na Mhe. Balozi Augustine Mahiga, Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, yalishuhudiwa pia na Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.