TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WASIFU WA
KATIBU
MKUU KIONGOZI MTEULE BALOZI MHANDISI JOHN KIJAZI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua
Balozi Mhandisi John William Kijazi (Pichani) kuwa Katibu Mkuu Kiongozi tarehe 6 Machi
2016, akichukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue.
Kabla
ya uteuzi huo, Balozi Mhandisi Kijazi alikuwa mwakilishi wa Tanzania nchini
India, Singapore, Sri Lanka, Bangladesh na Nepal mwenye makazi yake jijini New
Delhi, India kuanzia mwaka 2007 na hivyo kumfanya kuwa Mkuu wa Mabalozi wote
wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi. Vilevile, hadi uteuzi wake, Balozi Kijazi
amekuwa Mkuu wa Mabalozi wa Afrika nchini India ambaye amekuwa mtetezi mkuu wa
wanafunzi wenye asili ya Kiafrika nchini India.
Kabla
ya kuwa balozi, Mhandisi Kijazi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na baadaye
Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu kuanzia mwaka 2002 hadi 2006, baada ya
kuteuliwa kuwa Balozi ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa na hatimaye kupangiwa kituo cha New Delhi, India.
Kati
ya mwaka 1996 hadi 2002, Mhandisi Kijazi alikuwa Mhandisi Mwandamizi wa Ujenzi
wa Barabara ndani ya Wizara ya Ujenzi kabla ya kupandishwa cheo na kuwa
Mkurugenzi wa Barabara za Mikoa ndani ya Wizara hiyo hiyo.
Balozi
Mhandisi Kijazi alipata Shahada ya Sayansi ya Uhandisi wa Umma mwaka 1982
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, na baadaye Shahada ya Uzamili katika
Uhandisi wa Barabara Kuu kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza mwaka
1992.
Balozi
Mhandisi John Kijazi amemuoa Fransiscar Kijazi na pamoja wamejaliwa watoto watatu,
David, Emmanuel na Richard Kijazi.
Balozi
Mhandisi John Kijazi ataapishwa leo tarehe 7 Machi 2016 na Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu jijini Dar es salaam.
-MWISHO-
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara
ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda
na Kimataifa,
07 Machi 2016
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.