Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka kulia akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Brazil nchini Mhe. Carlos Alfonso Iglesia Puente, mazungumzo ambayo yalifanyika leo katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Katika mazungumzo hayo Mhe. Balozi alieleza kuwa Serikali ya Brazil katika kuimarisha ushirikiano na Tanzania itafadhili miradi ya kilimo katika Mkoa wa Simiyu kwa upande wa Tanzania, mradi ambao utakuwa na gharama ya Dola za Kimarekani milioni tano na lengo la mradi huo ni kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji kwa kutumia teknolojia za kisasa za kilimo hasa katika zao la Pamba ambalo ndio zao kuu la kilimo Mkoani humo ili kuliongezea thamani
Mhe. Mtaka katika mazungumzo hayo alipata nafasi ya kueleza fursa nyingine za uwekezaji zinazopatikana katika Mkoa huo ambapo alieleza licha ya kilimo cha pamba shughuli nyingine za kiuchumi ni uvuvi pamoja na ufugaji ambapo alieleza sehemu kubwa ya wakazi wa Mkoa huo ni wafugaji wa ng'ombe na kwamba kitaifa ni mkoa wa tatu kwa ufugaji wa ng'ombe
Wakati mazungumzo yakiendelea
Wakiagana mara baada ya mazungumzo
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.