TAARIFA
KWA UMMA
Sekretariati
ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imetangaza nafasi
mbalimbali 16 za ajira kupitia tangazo lao lililotolewa
tarehe 16 Aprili, 2016 Kumb. Na. SADC/2/3/3/3 katika tovuti ya http://www.sadc.int
Hata
hivyo, kulingana na utaratibu wa “quota points” kwa ajira za Sekretariati, kila
nchi mwanachama ana jumla ya pointi 121 ambapo kwa Tanzania tumebakiza pointi 5
tu. Pointi hizi hazitoshi kwa wananchi wetu kufanya maombi ya aina yoyote ya
ajira za Sekretariati kwa kipindi hiki.
Pointi
zinazohitajika kwa ajili ya kuomba nafasi ya ajira ni kuanzia pointi 12. Kwa
sababu hiyo, Tanzania haimo katika orodha ya nchi wanachama ambao wanakidhi
vigezo (eligible) kwa wakati huu.
Tunawaomba
Watanzania waendelee kutembelea tovuti ya SADC na tovuti ya Wizara kwa ajili ya
kupata taarifa kuhusu fursa zingine zitakazojitokeza.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa,
Dar es Salaam, 22 Aprili, 2016.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.