Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Korea chini Tanzania Mhe. Song, Geum-Young walipokutana na kufanya mazungumzo Wizarani Jijini Dar es Salaam. Mhe. Dkt. Kolimba katika mazungumzo hayo ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kuchangia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ikiwemo eneo la afya, elimu na teknolojia. Aidha amemuhakikishia Mhe. Balozi Young kuwa Wizara na Serikali kwa ujumla wataendelea kuboresha uhusiano mzuri wa Kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.