Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Mhe. Zehra Taskesenlioglu, Mbunge na Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wa Bunge la Uturuki wanaounda Kundi la Wabunge Marafiki na Wabunge wa Bunge la Tanzania alipofika Wizarani tarehe 23 Februari, 2018. Katika mazungumzo yao walizungumzia umuhimu wa kukuza na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Uturuki katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.