TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara, Viwanda,
Fedha na Uwekezaji
Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Kisekta
la Biashara, Viwanda, Fedha, na Uwekezaji unaendelea kufanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Masharik Jijini Arusha.
Mkutano huu unafanyika kwa muda wa siku tatu tarehe 7 hadi 9 Februari, 2018.
Pamoja na mambo mengine Mkutano huu unatarajiwa
kufanya mambo yafuatayo:
·
Kujadili kuhusu vikwazo vya biashara vya muda mrefu visivyo vya
kiushuru
·
Kupokea taarifa ya mwenendo wa sasa wa soko kati ya Umoja wa Ulaya
na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EU-EAC);
·
Kupokea taarifa ya Biashara na Uwekezaji ya mwaka 2016 ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki. Taarifa hii inaainisha mafanikio, changamoto na kutoa
mwenendo wa biashara na uwekezaji ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; na
·
Kupokea na kuridhia mwongozo wa Vituo vya Utoaji Huduma kwa Pamoja
Mpakani (OSBP) ambao utatoa utaratibu wa namna ya kuviendesha vituo hivyo
katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mkutano huu unafanyika ili
kujadili na kutoa ufumbuzi wa masuala mbalimbali kama ilivyoagizwa kwenye Mikutano
iliyopita ya Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mkutano huu
unafanyika katika ngazi tatu; ngazi ya Wataalamu, ngazi ya Makatibu Wakuu na
hatimaye katika ngazi ya Mawaziri.
-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
8 Februari 2018
Wajumbe kutoka Tanzania wakifuatilia Mkutano |
Sehemu ya Wajumbe kutoka nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki Wakifuatilia Mkutano |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.