Friday, March 2, 2018

Tanzania yashiriki Mkutano wa Kwanza wa Global Dryland Alliance

Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma M. Rajab (wa kwanza kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe walioshiriki mkutano wa kikao cha Kwanza cha Wajumbe wa Global Dryland Alliance. Balozi Rajab alimwakilisha  Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo. Mkutano huo ulifanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja iliyopo Doha, Qatar hivi karibuni. Umoja huo ambao ulianzishwa rasmi mwaka 2017  unaangalia namna ya kutatua majanga ya njaa yanayosababishwa na ukame, upungufu wa mvua na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kikao hicho kilizinduliwa rasmi na mwenyewe wa mkutano huo Mhe. Mohammed bin Abdullah Al Rumaihi Waziri wa Manispa na Mazingira wa Qatar. Na baadae kuendeshwa na Mwenyekiti mpya wa Umoja huo ambae pia ni Waziri wa Kilimo wa Benin.
Balozi Fatma M. Rajab akifuatilia  mkutano wa kikao cha Kwanza cha Wajumbe wa Global Dryland Alliance Tanzania ambapo alimwakilisha, Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo. Mkutano huo umefanyika Kwenye Makao Makuu ya Umoja huo yaliyopo Doha, Qatar. 
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea jengo jipya la Makao Makuu ya Global Dryland Alliance mjini Doha.




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.