TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri Mahiga afanya
mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Israeli
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amekutana na kufanya mazungumzo na
Waziri wa Ulinzi wa Taifa la Israeli Mhe. Avigdor Liberman. Mazungumzo hayo
yalifanyika katika ukumbi wa kupokelea wageni maalum(VIP) katika Uwanja wa
Ndege wa Julius Nyerere,Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Machi,2018.
Mazungumzo haya yalijikita zaidi katika
kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Israeli. Akiongea katika mazungumzo
hayo Waziri Mahiga alisema ziara hii ina maana kubwa sana kwa Tanzania na
itazidi kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizi mbili. Kama inavyofahamika nchi
ya Israeli ina Utaalam wa hali ya juu katika maeneo mbalimbali hasa katika masuala ya Ulinzi na Usalama,
Kilimo cha Umwagiliaji, mbinu za kisasa za kupambana na Ugaidi, Uhalifu wa Kimtandao na Teknolojia ya
tiba na vifaa tiba.
Naye Mhe. Liberman amesema
Israeli inaishukuru Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia kulinda
Amani ya Dunia hasa kwa kushiriki katika Ulinzi wa amani nchini Lebanon na nchi nyingine za afrika zenye migogoro, na
ameahidi nchi yake itaendelea kuongeza maeneo ya Mashirikiano zaidi na Tanzania.
Katika Ziara hii Mhe. Liberman
alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
John Pombe Magufuli, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt.
Hussein Mwinyi, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia,Wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na
Usalama.
Mhe. Liberman ameondoka tarehe 22 Machi, 2018, kurejea nchini
Israeli baada ya Ziara ya siku tatu(3) hapa nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo kwa Waziri wa Ulinzi wa Taifa la Israeli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Taifa hilo Mhe. Avigdor Liberman walipokutana kwa mazungumzo tarehe 22 Machi,2018, mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa kupokelea wageni Maalum(VIP) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Bw. Ayoub Mdeme na Bi. KisaDoris Mwaseba wakifuatilia mazungumzo hayo
Balozi wa Israeli nchini, ambaye Makazi yake yapo Jijini Nairobi Mhe. Balozi Noah Gal Gendler na Msaidizi wa Viongozi wakiwa katika mazungumzo hayo.
Waziri Mahiga akiagana na Mhe. Liberman baada ya kumaliza mazungumzo,
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.