Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta (BLM) la Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu unafanyika leo tarehe 9 Desemba 2021katika Hotel Verde mjini Zanzibar.
Mkutano huu na mkutano wa ngazi ya Maafisa Waandamizi ambao ulifanyika tarehe 6 hadi 8 Desemba 2021 ni sehemu ya mikutano ya awali yenye jukukumu la kupitia na kuwasilisha agenda na mapendekezo ya masuala ya afya ya kikanda yatakayo wasilishwa katika Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 10 Desemba 2021.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu unaongozwa na Dkt. Fatma H. Mrisho, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Viongozi wengine walioambatana naye ni pamoja na Dkt. Othman Mohamed Ahmed, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia - Tanzania Bara, Bw. Eliabi Chodota, Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Dkt. Abdul S. Ali, Mganga Mkuu na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mkutano huu unafanyika mjini Zanzibar kwa lengo la kuendeleza jitihada za jumuiya katika kutangaza maeneo ya utalii ndani ya jumuiya. Vilevile kuvutia wageni na kuhamasisha utalii wa ndani kama ilivyosisitizwa katika maonesho ya Utalii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC-Tourism Expo) yaliyofanyika mapema mwezi Oktoba 2021 Jijini Arusha.
==============================
Ujumbe wa Tanzania |
Ujumbe wa Tanzania |
Ujumbe wa Tanzania |
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Tanzania |
Ujumbe kutoka Kenya |
Ujumbe kutoka Uganda |
Ujumbe kutoka Burundi |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.