Na Mwandishi wetu, Dar
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) amepokea Hati za Utambulisho za Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula na
Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt. Nyabenyi Tipo katika Ofisi ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam.
Mara
baada ya kupokea hati hizo Balozi Mulamula ametumia fursa hiyo kumweleza
Mkurugenzi Mkazi huyo vipaumbele vya Serikali katika mpango mzima wa kuendeleza
kilimo pamoja na mpango Mkakati wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ‘Strategic
Development Cooperation programme’.
Pia
viongozi hao wameangalia maeneo ambayo yatapewa kipaumbele katika uwekezaji wa
miundombinu, uzalishaji zaidi lakini pia kuangalia jinsi gani mazao yanayolimwa
yanatunzwa vizuri.
“Tumejadili
mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpango wa FAo wa kusaidia nchi kuwa na bidhaa
zinazozitambulisha nchi husika katika masoko ya kimataifa,” amesama Balozi
Mulamula.
Pamoja
na mambo mengine, Balozi Mulamula amemhakikishia Mkurugenzi Mkazi wa FAO kuwa Tanzania
itaendelea kushirikiana kwa karibu na FAO katika kutekeleza miradi mbalimbali
hasa mradi wa maendeleo wa miaka mitano.
Kwa
Upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa
Mataifa (FAO) Dkt. Nyabenyi Tipo amesema atahakikisha FAO inatekeleza
vipaumbele vya Serikali ya Tanzania pamoja na kuongeza ushirikiano wake kwa
maslahi ya pande zote mbili.
“Mara
baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, tumejadili jinsi ya kusaidia kupunguza athari
za mabadiliko ya tabia nchi, kupunguza utapiamlo na kuona ni jinsi gani FAO
inaweza kusaidia Tanzania katika kuboresha lishe kwa watanzania na changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta ya kilimo kwa ujumla,” amesema Dkt. Tipo
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akipokea Hati za Utambulisho za Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula na
Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt. Nyabenyi Tipo katika Ofisi ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt. Nyabenyi Tipo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt. Nyabenyi Tipo akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula mara baada ya kumkabidhi Hati za Utambulisho katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt.
Nyabenyi Tipo wakiwa katika picha ya pamoja na badhi ya maafisa kutoka Wizarani
pamoja na Ofisi za FAO
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.