Baraza la
Katiba la Wizara ya Mambo ya Nje linatarajiwa kukutana leo kuanzia saa 4 asubuhi hii
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, mjini Dar es Salaam.
Wajumbe wapatao
100 wanatarajiwa kuhudhuria Mkutano huo wakiwemo viongozi wa Wizara, Wakurugenzi na Maafisa kutoka
Wizarani,wawakilishi kutoka Taasisi ya Chuo cha Diplomasia -Kurasini (CFR),
wawakilishi kutoka Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa - Arusha (AICC) na
Waheshimiwa Mabalozi Wastaafu wapatao 43 na Waziri wa Mambo ya Nje mstaafu Mzee
Ibrahim Kaduma.
Mgeni rasmi
atakuwa Mjumbe wa Tume ya Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe Dk. Salim Ahmed
Salim.
Aidha,
ripoti ya mwisho ya maoni hayo itawasilishwa rasmi kwenye Tume ya Katiba.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.