Thursday, August 22, 2013

Mhe. Membe apokea Magari ya msaada ya kubebea wagonjwa kutoka Korea Kusini


Magari ya wagonjwa yalitolewa na Korea Kusini kwa ajili ya majimbo ya vituo vya afya vinne vya majimbo ya Ruangwa na Nchinga Mkoani Lindi.

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akionyesha funguo ya moja ya magari ya msaada mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Mhe. Chung IL.
 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akipungia mkono watu waliohudhuria hafla ya makabidhiano huku akiendesha moja ya magari ya msaada kutoka Korea Kusini. 
 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa pili kutoka kushoto akimpa funguo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa), Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) ambaye jimbo lake la Ruangwa limepatiwa magari mawili.
 

Mhe. Kassim Majaliwa akifungua mlango wa  moja ya magari aliyokabidhiwa kwa ajili ya jimbo lake ili alijaribu.
 

Mbunge wa Nchinga, Mhe. Said Mtanda naye akijaribu moja ya magari aliyokabidhiwa kwa ajili ya wananchi wa jimbo lake la Nchinga.
 

Mhe. Membe kushoto akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Korea Kusini kabla ya shughuli ya kukabidhiana magari ya msaada.
 

Mhe. Naibu Waziri wa TAMISEMI wa kwanza kushoto, Mbunge wa Nchinga wa pili kutoka kushoto pamoja na Diwani wa moja ya Kata ya jimbo la Ruangwa wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Balozi wa Korea Kusini. (hawapo pichani)
 

picha ya pamoja
 


Balozi wa Korea Kusini wa kwanza kulia akibadilishana mawazo na Bw. Khatibu Makenga wa kwanza kushoto Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakati wa hafla hiyo.
 
picha na Ally Kondo

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.