Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akizungumza wakati wa kikao chake na Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda wa Afrika Kusini, Mhe. Elizabeth Thabethe (wa pili kushoto). Mhe. Thabete anaongoza ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Afrika Kusini utakaoshiriki Semina kuhusu Biashara na Uwekezaji itakayofanyika hapa nchini tarehe 23 Januari, 2014. Wengine katika picha ni Mhe. Radhia Msuya (kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini na Mhe. Thanduyise Chiliza, Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.