Waziri Mkuu wa Finland akitoa mada katika kikao maaulum kilichofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro. Kikao hicho kilijadili mbinu ambazo nchi za Afrika na Ulaya zikishirikiana kwa pamoja, zinaweza kuzitumia kukuza uchumi kwa faida ya wananchi wao. Katika mada yake Waziri Mkuu alisisitiza umuhimu wa kuimarisha Jumuiya za Kikanda kwa ajili ya kuleta maendeleo ya kiuchumi na utulivu wa kisiasa. Wazungumzaji wengine walisisitiza umuhimu wa Afrika na Ulaya kuwa na ushirikiano wenye uwiano sawa ambao utaleta maendeleo ya kiuchumi kwa pande zote mbili bila kudhulumiana. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.