Sunday, January 5, 2014

Viongozi wa Serikali wajumuika kutoa mkono wa pole na kuuaga mwili wa Dkt. William Mgimwa


Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiweka saini Kitabu cha Maombolezo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. William Mgimwa, wakati wa kutoa heshima za mwisho leo kwenye Viwanja vya Karimjee Hall, jijini Dar es Salaam.  (Picha na Ikulu)

Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimfariji mjane wa marehemu na familia yake. (Picha na Ikulu)

Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisaini Kitabu cha Maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. WilliamMgimwa, nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jana jijini Dar es Salaam.  (Picha na OMR)


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Bibi Jane Katingo, Mama Mzazi wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa, wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu huyo kutoa mkono wa pole leo na kuangalia maandalizi ya mazishi katika Kijiji cha Magunga, Iringa.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mhe. Waziri Bernard K. Membe (Mb) (wa pili kushoto), wakiwa wamebeba sanduku lenye mwili wa marehemu Dkt. William Mgimwa leo kwenye Viwanya vya Karimjee Hall, jijini Dar es Salaaam.  Mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumatatu tarehe 6 Januari, 2014 Mkoani Iringa. (Picha na Ikulu)


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.