Waziri Mkuu wa Finland kuzuru Tanzania
Waziri
Mkuu wa Findland, Mhe. Jyrki Katainen atafanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini
Tanzania tarehe 29 na 30 Januari, 2014.Mhe.Katainen anategemewa kuwasili usiku wa
tarehe 28 januari akitokea Addis Ababa, Ethiopia, na atafanyiwa mapokezi rasmi na
mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete,
kesho yake asubuhi.
Mhe. Katainen
atafuatana na Waziri wake wa Maendeleo ya Kimataifa, Mhe. Pekka Haavisto, na wafanyabiashara
25 wa Finland.
Baada
ya mapokezi rasmi, Mhe. Waziri Mkuu wa Finland atafanya mazungumzo na Mwenyeji
wake, Rais Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam, na baadaye atashiriki majadiliano kuhusu
ushirikiano kati ya Ulaya na Afrika, yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwenye hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro.
Wakati
wa ziara hiyo, Tanzania na Finland zitatiliana saini Mkataba wa Msaada wa Bajeti
(General Budget Support) na Makubaliano ya Ushirikiano (Memorandum of
Understanding) kwenye Nyanja za madini na misitu.
Mhe.Rais
Kikwete atamwandalia mgeni wake chakula rasmi cha jioni, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 29 Januari, Mhe. Katainen anatarajiwa kuzuru Unguja na kukutana na Rais wa Zanzibar, Mhe.
Dkt. Ali Mohamed Shein. Kadhalika, atafanya mazungumzo na Wafanybiashara,
wachumi na maafisa wa mashirika ya kimataifa jijini Dar es Salaam, pamoja na kutembelea
bandari, kabla ya kuondoka nchini Januari 30 usiku.
IMETOLEWA NA WIZARA YA
MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
DAR ES SALAAM, JANUARI 27,
2014
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.