Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim akipokea Tuzo ya Juu ya Umoja wa Afrika ya Mwana wa Afrika kwa Mwaka 2014 kutoka kwa Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, Mhe. Balozi Smail Chergui. Tuzo hiyo ilitolewa mjini Arusha pembezoni mwa Warsha ya Tano ya Ngazi ya Juu kuhusu Amani na Usalama Bararani Afrika iliyoandaliwa na Umoja wa Afrika inayoendelea mjini humo. Tuzo hiyo pia imetolewa kwa Balozi Mstaafu na Mpigania Uhuru Mahiri Barani Afrika, Balozi Hashim Mbita. Tuzo hizo zimetolewa kwao kutokana na mchango mkubwa walioutoa Barani Afrika na kwa Umoja wa Afrika ambapo Dkt. Salim alikuwa Katibu Mkuu wa saba wa OAU kuanzia mwaka 1989 hadi 2001. Kwa upande wake Balozi Mbita alikuwa Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Ukombozi Barani Afrika chini ya OAU kuanzia mwaka 1974 hadi 1994 ilipomaliza kazi yake baada ya Uhuru wa Afrika Kusini. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.