Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Celestin Tunda ya Kasende alipofika Wizarani kwa ajili ya mazungumzo kuhusu masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na DRC. Katika mazungumzo hayo Mhe. Tunda ya Kasende aliishukuru Serikali ya Tanzania na Watanzania kwa ujumla kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha amani inarejea DRC. Mhe. Tunda ya Kasende pamoja na ujumbe wake yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.