Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bw.John Haule (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa
Mataifa tarehe 21 hadi 25 Oktoba, 2014.
Wiki hiyo ambayo huadhimishwa kila mwaka itajumuisha gwaride rasmi na kupandishwa bendera katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam tarehe 24 Oktoba. Sherehe hizo zitahitimishwa na bonanza la michezo mbalimbali litakalo husisha wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje kwenye viwanja vya Gymkhana tarehe 25 Oktoba. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni "Agenda ya Maendeleo baada ya
2015 - Asiachwe mtu nyuma (The Post 2015 Development Agenda - leaving No one
Behind)". Wakwanza kushoto ni Bwa. Alvaro Rodriguez, Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini, na wakwanza kulia ni
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.