Mhe. Balozi Migiro akifurahia jambo na sehemu ya Watanzania walioshiriki uzinduzi huo |
Sehemu ya Watanzania na wageni waalikwa waliohudhuria tukio hilo la kihistoria |
===================================================
UZINDUZI WA ASSOCIATION OF TANZANIANS IN
THE UK – ATUK
Mhe. Dkt.
Asha-Rose Migiro, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, alikuwa mgeni rasmi
kwenye sherehe za uzinduzi wa Jumuiya Mwamvuli ya Watanzania waishio nchini
Uingereza na Ireland ya Kaskazini iitwayo ATUK –Association
of Tanzanians in the UK zilizofanyika mjini Reading tarehe 23
Juni, 2018. Jumuiya hii inatokana na muungano wa jumuiya za diaspora kutoka
mikoa mbalimbali ya hapa Uingereza na wanachama wa kujitegemea.
Wajumbe
wa Kamati ya Muda iliyoratibu kuanzishwa kwa ATUK walipongeza
na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za
kupambana na ufisadi, kusimamia uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma na
kuongeza kasi ya kujenga uchumi wa viwanda. Kauli mbiu ya hafla hii ilikuwa
“UMOJA NI NGUVU, TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA”. Hivyo mojawapo ya malengo ya
kuanzishwa kwa ATUK ni kujenga umoja na kukusanya nguvu za kuchangia jitihada
za kujenga uchumi wa viwanda nchini mwetu.
Akihutubia
hadhara hiyo Balozi Migiro aliwapongeza ATUK na
alihimiza umoja na kukumbusha kwamba wakati wote Mhe. Rais amekuwa akisisitiza
umoja wa Watanzania bila kujali tofauti zao kwani umoja ni nyenzo muhimu ya
kujiteletea maendeleo. Hivyo Balozi Migiro aliwashukuru kwa Muungano huo na
kueleza kwamba wakiendeleza mshikamano wataweza kuchangia kwa
ufanisi jitihada kubwa za Mhe. Rais Magufuli na Serikali ya Awamu ya
Tano katika kuwaletea maendeleo Watanzania wote.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.