Mhandisi Abdillah Mataka Mkurugenzi Msaidizi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Kijamii kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akichangia jambo kwenye mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa unaoendelea jijini Arusha. Mkutano huu unafanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano huu unaofanyika kila mwaka, mwaka huu pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili taarifa za utelelezaji wa mapendekezo, maagizo na maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na kuamuliwa katika mikutano ya ngazi mbalimbali na vyombo vya kisera vya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Sekta zinazotarajiwa kujadiliwa katika mkutano huu ni pamoja na sekta ya miundombinu ya uchukuzi inayojumuisha aridhi, anga na maji, mawasiliano na hali ya hewa.
Utelezaji wa maagizo, mapendekezo na maamuzi mbalimbali yaliyotolewa ili kuboresha maeneo haya unatarajiwa kuleta mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii katika nchi wanachama za Jumuiya Afrika Mashariki.
Mkutano huu unaoendelea jijini Arusha na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi zote wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki utafanyika katika ngazi tatu ambazo ni; ngazi ya Wataalam, ngazi ya Makatibu Wakuu na hatimaye ngazi ya Mawaziri.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.