Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda (kulia) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini, Bw. Michael Dunford alipofika Wizarani kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa majukumu unaofanywa na Shirika hilo hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Mwakilishi huyo aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa anaopata katika kutekeleza majukumu yake. Shirika la WFP hapa nchini linajishughulisha katika kusaidia miradi mbalimbali ya kilimo katika kuwajengea uwezo wakulima wadogo, lishe na kusaidia upatikanaji wa soko kwa wakulima wadogo. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.