Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan M. Mwinyi, akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Poland nchini Mhe. Krzysztof Buzalski alipomtembelea Wizarani tarehe 07 Juni,2018, Dar es Salaam,
Mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine yalijikita katika kuboresha mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na Poland. Balozi Mwinyi alisema Poland ni kati ya nchi ambazo Mahusiano yake yameleta manufaa katika nyanja mbalimbali za uchumi hapa nchini, hasa katika eneo la kuendeleza kilimo cha kisasa. Itakumbukwa hivi karibuni nchi ya Poland imetoa mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi wa maghala yanayotumia teknologia ya kisasa kuhifadhi nafaka katika Mikoa mitano(5) hapa nchini.
Naye Balozi Buzalski alisema Poland inafurahishwa na Juhudi za Serikali ya awamu ya tano(5) ya Kujenga Tanzania ya Viwanda na amesema kilimo ni kati ya eneo muhimu ambalo litasaidia Tanzania kufikia adhma hiyo kwa haraka ndio maana wameamua kuongeza nguvu kwenye eneo hili nyeti.
Ili kuwajengea uwezo Watanzania Poland imefungua tena fursa za masomo nchini humo katika
maeneo mbalimbali hivyo Watanzania wanashauriwa kuchangamkia fursa hizo
zitakapotangazwa .
Aidha, Balozi Buzalski pia amesema eneo lingine muhimu ni katika sekta ya utalii ambapo hadi sasa watalii kutoka Poland wameongezeka maradufu ambapo jumla ya watalii 12,000 kutoka Poland wanatembelea Tanzania kwa Mwaka na kati ya hao Watalii 10,000 wanaenda Zanzibar.
Mkutano ukiendelea, wanofuatilia kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Europe na Amerika Bi Mona Mahecha na kushoto ni Naibu Balozi wa Poland Bi.Awelina Lubieniecka.
Balozi Mwinyi akiagana na mgeni wake Balozi Buzalski baada ya mazungumzo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.