Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi awasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa Fedha 2020/2021.
Wizara imeliomba Bunge liiidhinishie
jumla ya Shilingi bilioni mia moja
tisini na tisa, milioni mia saba hamsini, laki sita themanini na nne elfu (199,750,684,000) zikiwa ni fedha kwa ajili ya
Matumizi ya Kawaida na bajeti ya miradi ya maendeleo.
Akiwasilisha makadirio hayo, Mhe. Prof. Kabudi ameelezea mafaniko ambayo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeyapata katika kipindi hiki cha kwanza cha Serikali ya Awamu ya Tano 2015-2020.
Mafanikio hayo ni:
* Ufunguzi wa Balozi mpya nane katika nchi za Qatar; Uturuki; Sudan; Cuba; Israel; Algeria; Jamhuri ya Korea; na Namibia;
* Kuifanya lugha ya
Kiswahili kutumika katika Jumuiya ya Kimataifa na nchi mbalimbali;
* Kufanikisha kufanyika
kwa viwango vya juu Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Dar es Salaam mwezi Agosti 2019;
*Kuhamasisha watalii kuja
nchini kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii;
*Kufanikisha uenyekiti
wa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo mwezi Machi 2016 nchi yetu iliteuliwa kwa mara
ya pili mfululizo kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo;
*Kuratibu Mkutano wa 18
wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika na Nordic
(Africa - Nordic Foreign Ministers’ Meeting) uliofanyika kwa mafanikio makubwa
mwezi Novemba 2019 jijini Dar es Salaam;
*Kufanikisha
ujumuishwaji wa miradi ya Tanzania katika miradi ya kipaumbele ya miundombinu
iliyoidhinishwa na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki;
*Kutekeleza
Itifaki ya Umoja wa Forodha na Itifaki ya Soko la Pamoja za Jumuiya ya Afrika
Mashariki;
Mafanikio mengine ni pamoja na;
*Kuratibu upatikanaji
wa mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya
Maendeleo Afrika (AfDB) wenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 200 kwa ajili
ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato jijini Dodoma na upatikanaji
wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 180
kutoka Benki hiyo kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya pete katika jiji la Dodoma na
* Kushawishi nchi marafiki kutufutia madeni, kuyapunguza au kuweka masharti nafuu ya kuyalipa.
* Kushawishi nchi marafiki kutufutia madeni, kuyapunguza au kuweka masharti nafuu ya kuyalipa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.