Serikali
ya Tanzania imewarejesha nchini watanzania 119 ambao walikuwa wamekwama Abu
Dhabi (Dubai) kufuatia kuzuiwa kwa safari za ndege kutokana na mlipuko wa
ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosabishwa na virus vya corona (COVID-19).
Ndege
ya fly Dubai imewarejesha watanzania hao waliokuwa wamekwama Abu Dhabi (Dubai) tangu
25 Machi 2020 Serikali ya Falme za Kiarabu ilipotoa zuio la kuingia na kutoka kwa
ndege.
Ndege
hiyo imewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa
8 mchana leo Alhamisi tarehe 21 Mei 2020 ikiwa na watanzania 119.
Kabla
ya ndee hiyo kuwasili katika uwanja wa ndee wa Kimataifa wa Julius Nyerere,
wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wa watanzania hao walionekana wakiwa na nyuso
za furaha na shauku ya kuonana na ndugu zao.
"Tunashukuru
Serikali yetu ya Tanzania kwa kuweza kuturejesha nyumbani….binafsi namshukuru
sana sana Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi za kuturejesha, pia naushukuru
ubalozi wa Tanzania katika Falme za Kiarabu kwa msaada wa hali na mali pamoja
na nchi ya Falme za Kiarabu na watanzania kwa umoja na upendo kwani wengine
tulikuwa hatuna fedha ya tiketi lakini kwa umoja tumeweza kuchangiwa na kurejea
tena nchini kwetu," Amesema Mohhamed Juma Omary.
Kwa
Upande wake, Bi. Christina Magige ambaye alikuwa amekwama Dubai kwa miezi mitatu
ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Falme za
Kiarabu kwa kuweza kutoa ndege ambayo imeweza kuwarejesha nyumbani.
"Nampongeza
sana Serikali yanu ya Tanzania kwa kuweza kufungua viwanja vya ndege ambapo kwa
kufanya hivyo imetusaidia sisi watanzania tuliokuwa nje ya nchi kuweza kurejea
nchini leo tunamshukuru sana, amesema bi. Magige.
Tarehe
15 Mei, 2020 jumla ya watanzania 246 waliokuwa wamekwama katika miji mbalimbali
nchini India kutokana na zuio la kuingia na kutoka ndege za Kimataifa
lililowekwa na Serikali ya India kama hatua mojawapo ya kudhibiti kuenea kwa
maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 walirejea nchini.
Ndege
ya flydubai iliyowarejesha watanzania 119 nchini kutoka Abu Dhabi (Dubai) ikitua
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo jijini Dar es
Salaam
|
Baadhi
ya watanzania waliokuwa wamekwama Dubai wakishuka kwenye ndege ya flydubai mara
baada ya ndee iyo kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
leo jijini Dar es Salaam
|
Baadhi
ya watanzania waliokuwa wamekwama Dubai wakishuka kwenye ndege ya flydubai mara
baada ya ndee iyo kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
leo jijini Dar es Salaam
|
Baadhi
ya watanzania waliokuwa wamekwama Dubai wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo jijini Dar es Salaam
|
Baadhi
ya watanzania waliokuwa wamekwama Dubai wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo jijini Dar es Salaam
|
Baadhi
ya watanzania waliokuwa wamekwama Dubai wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo jijini Dar es Salaam
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.