Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Mhe.
Roberto Mengoni katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo
hayo pia yalihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, ambapo walijadili masuala
mbalimbali yanayohusu mahusiano baina ya Tanzania na Italia.
Aidha,
walitumia mazungumzo hayo kujadili hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali
ya Tanzania pamoja na Serikali ya Italia katika kupambana na ugonjwa wa
COVID-19. Mhe. Waziri alifahamisha kuwa hatua mbalimbali zilizochukuliwa na
Serikali ya Tanzania kwenye mapambano ya ugonjwa huo zimezingatia mazingiria na
hali halisi ya Tanzania pamoja na nchi jirani zinazozunguka Tanzania.
Kwa
upande wake Balozi Mengoni alipongeza juhudi hizo za Serikali ambapo
alifahamisha kuwa Serikali yake ya Italia inaziunga mkono na kwamba ipo tayari
kutoa ushirikiano pale itakapohitajika kufanya hivyo.
Viongozi
hao walikubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kihistoria baina ya
Mataifa hayo mawili ambao umejikita katika sekta za elimu, afya, utalii pamoja
na biashara na uwekezaji.
Balozi
wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali
Wilbert A. Ibuge
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John
Kabudi akimuelezea jambo Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni pamoja na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Kanali Wilbert A. Ibuge
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.