Ubalozi
wa Tanzania nchini India, kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Tanzania [Air
Tanzania] pamoja na Diaspora wa Tanzania nchini India wamefanikisha safari ya
kwanza ya kuwarejesha nchini watanzania waliokuwa wamekwama katika miji
mbalimbali nchini India kutokana na zuio la kuingia na kutoka ndege za
Kimataifa lililowekwa na Serikali ya India kama hatua mojawapo ya kudhibiti
kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19.
Ndege
maalum ya Boeng 787-8 ya Dreamliner ya Air Tanzania ilitumwa na Serikali Jijini
Mumbai kwenda kuwachukua watanzania hao waliokwama nchini India tangu tarehe 22
Machi 2020 lilipowekwa zuio hilo na Serikali ya India. Ndege hiyo imeondoka
India leo tarehe 15 Mei 2020 saa 2 asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Chhatrapati Shivaji International
Airport, Mumbai ikiwa imebeba jumla ya raia wa Tanzania 246, miongoni mwao ni
waliokuwa wameenda India kwa ajili ya matibabu, wahitimu kutoka vyuo mbalimbali
na wanafunzi ambao wanalazimika kurudi nyumbani kwa kuwa vyuo vimefungwa hadi
mwezi Agosti/Septemba 2020.
Ndege
hiyo imewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere [JNIA]
mnamo saa 6 mchana leo Ijumaa tarehe 15 Mei 2020. Takriban watanzania 410
walijiandikisha katika Ubalozi wa Tanzania, New Delhi na kuelezea utayari wao wa kuchangia gharama.
Kwa
kuwa idadi ya watanzania waliojitokeza ilikuwa kubwa zaidi ya waliweza kusafiri
katika awamu hii ya kwanza, Serikali inaangalia uwezekano wa kutuma ndege
nyingine maalum ya Air Tanzania kuja kuwachukua raia waliosalia ndani ya mwezi
huu. Gharama ya tiketi ya ndege hiyo, namna ya kulipa, Mahali ambapo ndege
itatua pamoja na tarehe za kuwasili kwa ndege hiyo nchini India zitatangazwa na
Ubalozi mapema iwezekanavyo.
Ubalozi
unapenda kuwashukuru Diaspora wa Tanzania nchini India kwa kufanikisha zoezi
hili kwa weledi mkubwa na Uongozi wa Wizara za Mambo ya Nje za India na
Tanzania na Serikali, kwa ujumla, kwa miongozo mbalimbali wakati wa zoezi hili.
Kabla
ya ndee hiyo kuwasili katika uwanja wa ndee wa Kimataifa wa Julius Nyerere
wazazi, nduu na jamaa wa watanzania hao walionekana wakiwa na nyuso za furaa huku
wakiwasubiria ndugu zao.
Mmoja
kati ya wanafunzi waliokuwa wanasoma India, Sulemani Khalidi ameishukuru sana
Serikali kwa kuwarejesa…. “Kwa kweli naishukuru sana Serikali yangu
kwa kusirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kutusaidia sisi sote hadi
kufika hapa nchini leo,”. Amesema Khalidi
Baadhi wa watanzania wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere [JNIA] wakitokea nchini India |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.