Serikali
ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
imesema changamoto zinazojitokeza katika mipaka mbalimbali ya Tanzania wakati
wa usafirishaji wa bidhaa hususan katika kipindi hiki cha janga la COVID-19
zinaendelea kutatuliwa kwa majadiliano.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali
Wilbert Ibuge ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa
Tanzania Nchini Zambia Mhe. Benson Keith Chali ili kuangalia namna ya kutatua
changamoto mbalimbali za usafirishaji wa bidhaa hususani zile zinazotoka katika
bandari ya Dar es Salaam kuelekea katika nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika SADC.
Ameongeza
kuwa katika kipindi hiki cha janga la COVID – 19 unaosababishwa na virusi vya
Corona changamoto mbalimbali zimejitokeza katika utoaji wa huduma za
usafirishaji wa huduma na bidhaa mbalimbali na hivyo serikali inafanya jitihada
za majadiliano na baadhi ya nchi katika mipaka ili kutatua changamoto
zinazojitkeza na kuwezesha huduma ya usafirishaji kuendelea bila ya vikwazo.
Nae
Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mhe. Chali amemuahidi Balozi Kanali Ibuge
kuwa Serikali ya Zambia imeshaanza kuzifanyia kazi changamoto zinazojitokeza.
"Suala hili limeshaanza kufanyiwa kazi na kila kitu kitakuwa sawa hivi
karibuni," amesema Balozi, Chali.
Katika
tukio jingine Balozi Kanali Wilbert Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo na
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bi.
Christine Musisi ambapo katika mazungumzo hayo wameongelea zaidi namna ya
kushirikiana na kuwezesha kujenga uwezo wa kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa
wawekezaji wadogo na wakati wa Tanzania na kuwa na ubia na wawekezaji wakubwa
hususani katika kipindi hiki cha COVID – 19 na baada ya COVID – 19 ili
kuunusuru uchumi wa Taifa kuanguka.
"Tumekubaliana
kuongea ushirikiano katika sekta za afya, maji, maendeleo na uwekezaji …….kwa
hili tunawashukuru sana UNDP kwa kazi wanayoifanya lakini pia hata katika
ushirikiano wa kisera tumekuwa tukishirikiana nao jambo ambalo linazidi
kuimarisha uhusiano wetu hasa katika wakati huu wa COVID - 19 kwani jambo hili
linasaidia kunusuru uchumi wa taifa kuanguka," amesema Balozi, Kanali
Ibuge.
Katika
hatua nyingine, Balozi Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo kwa nyakati
tofauti na Balozi wa Uingereza nchini Bi. Sarah Cooke pamoja na Mratibu Mkazi
wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania Bw. Zlatan Milišić ambapo wamezungumzia
masuala mbalimbali ya ushirikiano hususani katika kipindi hiki cha janga la
COVID – 19.
Tarehe
6 Aprili, 2020 ulifanyika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya
ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano
huo ulijadili janga la COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona. Mkutano
huo ulihusisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Fedha,Viwanda,Biashara, Utalii, Mambo ya Ndani na Uchukuzi, kutoka
nchi 16 wanachama wa SADC.
Katika
mkutano huo, Baraza la Mawaziri lilitoa mwongozo kuhusu Usafirishaji wa Bidhaa
Muhimu na Huduma katika Nchi za SADC katika kipindi hiki cha janga la Virusi
vya Corona. Mwongozo huu unatumika katika kipindi hiki unalenga kupunguza safari
zisizo za lazima na kuwezesa usafirishaji wa bidhaa muhimu wakati huu wa janga
la COVID - 19.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge akimueleza jambo Balozi wa
Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke wakati walipokutana kwa mazungumzo leo jijini
Dar es Salaam
Balozi wa Uingereza nchini Mhe.
Sarah Cooke akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge wakati walipokutana kwa
mazungumzo leo jijini Dar es Salaam
Balozi wa Zambia nchini Mhe. Benson
Keith Chali akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge wakati walipokutana kwa
mazungumzo leo jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge akiongea na
Balozi wa Zambia nchini Mhe. Benson Keith Chali leo jijini Dar es Salaam
Mratibu Mkazi wa Shughuli za
Umoja wa Mataifa (UN), Bw. Zlatan Milišić akimuelezea jambo Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge
wakati walipokutana kwa mazungumzo leo jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge akiongea na
Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN), Bw. Zlatan Milišić wakati
walipokutana kwa mazungumzo leo jijini Dar es Salaam
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Christine Musisi akimuelezea jambo
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali
Wilbert Ibuge wakati walipokutana kwa mazungumzo leo jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge akimfafanulia
jambo Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi.
Christine Musisi
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.