Katika jitihada za kuendeleza Diplomasia ya Uchumi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekubaliana na Jamhuri ya Namibia kuimarisha sekta za uvuvi na mifugo.
Makubaliano
hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) amekubaliana na Naibu
Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah kuimarisha
ushirikiano katika sekta ya Uvuvi pamoja na Sekta ya Mifugo.
"Tumekubalina kuimarisha ushirikiano katika
enao la uvuvi wa bahari kuu lakini pia kuwahamasisha wadau wa sekta binafsi
kutoka Tanzania na Namibia kuwekeza katika eneo hilo. Kwa upande wa mifugo na
uuzaji wa nyama nchi za nje Namibia wamepiga hatua kubwa sana na sasa wanauza
nyama Ulaya na Asia," Amesema Prof. Kabudi
Aidha, Prof. Kabudi ameongeza kuwa wamekubaliana
pia kuhamasisha sekta binafsi kutoka Namibia kuja kuwekeza katika machinjio na
viwanda vya kusindika nyama hapa nchini (Tanzania) kwa ajili ya kuuza nyama
hiyo nje ya Tanzania na kuendeleza sekta za uvuvi na mifugo.
Pamoja na mambo mengine, kikao cha leo kimepitia
makubaliano ya miaka miwili iliyopita ambapo Tanzania na Namibia zimekubaliana
kutumia fursa zilizopo kati yao kuendeleza sekta za uwekezaji, uvuvi, kilimo na
mifugo kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.
Kwa upande wake Naibu
Waziri Mkuu Wa Jamhuri Ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah amesema
kuwa wamekubaliana kuimarisha sekta mbili ambazo ni Uvuvi na mifugo pamoja na
kilimo kwa ujumla kwa kuzingatia mazingira bora ya uwekezaji na biashara ndani
ya Umoja wa Afrika (AU).
"Kuna maeneo mbalimbali ambayo kwa pamoja
tumekubaliana kuyaimarisha ikiwemo uvuvi, mifugo na kilimo kwa ujumla, kupitia
kikao cha leo tunaamini kuwa wawekezaji kutoka Namibia watakuja kuwekeza
Tanzania na vilevile wawekezaji kutoka Tanzania watawekeza Namibia,"
Amesema
Ameeleza kuwa Namibia itaendelea kufanya kazi kwa
karibu na Tanzania katika kuhakikisha kuwa wanakuza uchumi wa nchi zetu zote
mbili na Afrika kwa ujumla kwa kuzingatia misingi ya biashara na uwekezaji
iliyopo ndani ya Umoja wa Afrika (AU).
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.