Wawekezaji kutoka nchini Uturuki wamewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kujionea fursa za uwekezaji na biashara zilizopo nchini ili waweze kuwekeza na kukuza Diplomasia ya Uchumi baina ya mataifa hayo.
Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo amethibisha kuwasili
kwa wawekezaji hao wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki "Compass
Partners" leo jijini Dar es Salaam, na kuongeza kuwa wawekezaji watano kati
ya kumi wamefika nchini na kujumika na waturuki wengine wanaofanya biashara zao
hapa nchini.
"Wawekezaji
hawa kutoka Uturuki wamekuja na wamefungua taasisi yao inayojulikana kwa jina
la "Compass Partners" ili kuendeleza biashara na tunaamini kwa
kutekeleza biashara hii tunaenda kuendeleza uchumi wa Tanzania na kutengeneza
ajira kwa watanzania," Amesema Prof. Kiondo
Prof.
Kiondo ameongeza kuwa, hatua ya kwanza wawekezaji hao wameleta bidhaa mbalimbali
ili watanzania wazione, hatua ya pili itakuwa ni uwekezaji wa kiwanda hapa
nchini kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa bidhaa ambazo zitauzwa hapa nchini.
Aidha,
kwa upande wa bidha zinazozalishwa hapa nchini ambazo zina fursa ya kuuzwa
Uturuki ni pamoja na chai, pamba, tumbaku na kahawa bidhaa hizi zote zina soko
kubwa sana nchini Uturuki.
Tunazalisha
tani 350,000 za pamba lakini tunaweza kuchakata asilimia 15 tu, hivyo tumepata
tayari mwekezaji ambaye atawekeza katika kiwanda cha nguo mkonani simiyu ili
kuongeza thamani ya bidhaa ya pamba hapa nchini.
Balozi,
Prof. Kiondo ametoa wito kwa Watanzania kuanza kuchangamkia fursa hizo za
biashara ili waweze kuongeza kipato na kuongeza biashara zao.
Kwa
upande wake, Kaimu Balozi wa Uturiki hapa Nchini, Mhe. Onur Yah amesema kuwa biashara
kati ya Tanzania na Uturiki imekuwa ikiimarika kila wakati kwani Tanzania ni
sehemu salama ya kuwekeza na kufanya biashara.
"Kupitia
uwekezaji katika sekta mbalimbali ni imani yangu kuwa tutaendelea kukuza na
kuimarisha uhusiano wetu wa kidiplomasia," Amesema Mhe. Yah
Aidha,
amewataka Waturuki na Watanzania kutumia fursa za biashara zinazopatikana baina
ya mataifa hayo ili kufanya biashara na kukuza uchumi wao.
Ushirikiano
wa Tanzania na Uturuki ni wa muda mrefu, pamoja na mambo mengine uhusiano huo
umekuwa ukijikita zaidi katika kuendeleza uwekezaji wa viwanda, elimu na utalii
hasa katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Uturuki.
Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akiongea na wanahabari
(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki "Compass
Partners" leo jijini Dar es Salaam
Kaimu
Balozi wa Uturiki hapa Nchini, Mhe. Onur Yah akiongea na wanahabari (hawapo
pichani) wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki "Compass Partners"
leo jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo pamoja na Kaimu Balozi
wa Uturiki hapa Nchini, Mhe. Onur Yah wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa
Taasisi ya Waturiki "Compass Partners" leo jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.