Na Mwandishi Wetu, Dar
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax ameishauri Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) kutumia teknolojia
vizuri katika kukuza na kuendeleza diplomasia ya uchumi pamoja na masuala ya
ulinzi na usalama
Dk.
Stergomena Tax ametoa ushauri huo wakati alipokuwa akifunga mafunzo maalumu ya
siku tano ya Wajumbe wa Kamati ya NUU yaliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo Jijini Dar es Salaam.
Pamoja
na mambo mengine, mafunzo hayo yamelenga kuwaongezea ujuzi wabunge ambao ni
wajumbe wa kamati hio katika masuala ya diplomasia ya uchumi, maslai ya taifa,
mawasiliano ya kidemokrasia, uchumi wa bluu, ushirikiano wa Kimataifa na usalama
wa nyaraka za kibalozi.
"Huwezi
ukatenganisha diplomasia na ulinzi na usalama hususani katika dunia ya sasa
ambayo ni dunia ya teknolojia, inayokuwa kwa kasi, diplomasia inatengemea
ulinzi na usalama, diplomasia inaongoza maslahi ya Taifa haya ni mambo ambayo
hayawezi kutenganishwa," amesema na kuongeza kuwa;
"Teknolojia
hii ni muhimu sana katika kuendeleza uchumi na masuala ya diplomasia, ulinzi na
usalama kama ikitumika vyema, ila ni vyema tukazitambua pande zote mbili wakati
tunatumia teknolojia hii tunalo jukumu ya kutuletea manufaa lakini pia tunalo
jukumu la kuwa walinzi wa rasilimali za Taifa letu,"
Awali
akimkaribisha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mwenyekiti wa Kamati
ya NUU Bw. Mussa Zungu amewasihi watanzania kubadilika na kujikita kujenga
uchumi imara.
“Uchumi
imara unahitaji diplomasia katika kusimamia maslahi mapana ya Taifa……………hatuwezi
kupigwa kama tutakuwa na watu imara
wanaopigania maslahi ya taifa letu, lazima sisi kama kamati inayo ‘cross-cut’ masuala
mengi tusimamie maslahi ya taifa letu” Amesema Mhe. Zungu
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Joseph Sokoine amesema Wizara itaendelea kuboresha mafunzo
mbalimbali kwa kamati ya NUU kwa lengo la kuwajengea uwezo na ujuzi katika
kutekeleza majukumu yao kadri dunia inavyo kwenda.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Bw. Mussa
Zungu (Mb) akitoa hotuba kwa wajumbe wa kamati anayoiongoza Jijini Dar es
Salaam
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax akihutubia Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) katika hafla ya
kufunga mafunzo maalumu kwa kamati hiyo Jijini Dar es Salaam
Wajumbe
wa Kamati ya NUU wakimsikiliza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.
Stergomena Tax (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.
Stergomena Tax akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Katai ya NUU mara baada ya kumaliza mafunzo maalumu yaliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.