Na Mwandishi wetu, Dar
Tanzania
na Ufaransa zimetajwa kuwa ni ujumbe wa utulivu, amani na maendeleo duniani na
kwamba tukio la hivi karibuni katika ubalozi huo halikuathiri kwa namna yeyote
mahusiano baina ya Nchi hizo.
Balozi
wa Ufaransa hapa nchini mhe. Frederic Clavier ameyasema hayo Jijini Dar es
Salaam alipokutana kwa mazungumzo pamoja na kumuaga Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) baada ya kumaliza
muda wake wa uwakilishi hapa nchini na kuongeza kuwa katika kipindi chote cha
utumishi wake ameiona Tanzania kuwa ni ujumbe wa utulivu,amani na maendeleo kwa
Bara la Afrika na duniani kwa ujumla.
“Katika
kipindi chote cha uwakilishi wangu hapa Tanzania, nimeiona Tanzania kuwa ni
ujumbe wa utulivu, amani na maendeleo kwa Bara la Afrika na duniani kwa ujumla,”
Amesema Balozi Clavier.
Balozi
Clavier ameongeza kuwa ushirikiano kati ya Ufaransa na Tanzania katika nyanja
mbalimbali za maendeleo ikiwemo elimu, afya, miundombinu biashara na uwekezaji
umeendelea kukua kwa kiwango kikubwa na kwamba Ufaransa itaendela kukuza
mahusiano hayo ya kihistoria baina ya nchi hizo mbili.
Ameongeza
kuwa Ufaransa itaendelea kutoa kipaumbele katika kuendeleza uchumi wa buluu
ambao kwa sasa umewekewa mikakati mahususi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kama chanzo kipya cha kuongeza mapato ya serikali lakini pia kupunguza
umasikini kwa Watanzania wote na kwamba anaporejea Ufaransa atahamasisha
makampuni, wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Ufaransa kuja
kuwekeza Tanzania.
Kwa
upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula (Mb) amemshukuru Balozi Frederic Clavier kwa kuimarisha na
kuendeleza mahusiano baina ya Tanzania na Ufaransa.
Balozi
Mulamula amempa pole Balozi huyo kwa tukio la kihalifu lililotokea hivi
karibuni katika Ubalozi wa Ufaransa na kumhakikishia kuwa licha ya tukio hilo
ambalo lilidhibitiwa na vyombo vya dola,Tanzania ni salama.
Balozi
wa Ufaransa aliyemaliza muda wa uwakilishi hapa nchini, Mhe. Frederic Clavier
akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Maongezi
baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Liberata Mulamula na Balozi wa Ufaransa aliyemaliza muda wa uwakilishi hapa
nchini, Mhe. Frederic Clavier yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini
Dar es Salaam
Maongezi
baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Liberata Mulamula na Balozi wa Ufaransa aliyemaliza muda wa uwakilishi hapa
nchini, Mhe. Frederic Clavier yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini
Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula
(Mb) akitoa zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro kwa Balozi wa Ufaransa
aliyemaliza muda wa uwakilishi hapa nchini, Mhe. Frederic Clavier
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.