Friday, April 13, 2018

Naibu Waziri akutana na kufanya mazungumzo na Spika EALA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Mhe. Martin Ngoga wakisalimiana walipokutana kwa mazumgumzo katika Ofisi za Wizara Dodoma.

Mhe. Ngoga alimtembelea Naibu Waziri Mhe. Dkt. Kolimba Ofisini kwake ambapo walifanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Jumuiya. Mhe. Dkt.Kolimba katika mazungumzo hayo amemwahidi Spika wa EALA kuwa Wizara na Serikali kwa ujumla itatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Bunge hilo katika utelezaji wa majukumu yake.

Aidha kwa upande wake Spika wa EALA amesema kuwa,kwa sasa wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanadumisha ushirikiano na Mabunge ya Nchi wanachama na kutoa mrejesho kwa Nchi wanachama kuhusu masuala mbalimbali ya yanayojili katika Bunge hilo.

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linafanya vikao vyake mjini Dodoma kuanzia tarehe 9 hadi 28 Aprili, 2018 

Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Mhe. Martin Ngoga akisaini kitabu cha wageni mara baada kuwasili Wizarani Dodoma. 
Naibu Waziri Mhe. Dkt. Kolimba na Spika wa EALA Mhe. Dkt.Ngoga wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wabunge wa EALA na Maafisa kutoka Wizarani na Bunge la EALA 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.