Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania nchini Kenya, Balozi Anisa Mbega walipokutana na Wadhamini na Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya maonesho hayo (hawapo pichani) yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 25 - 28 Aprili 2018 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi, Kenya.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 12 Aprili 2018 katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam na kuambatana na hafla ya kukabidhi udhamini kwa ajili ya kufanikisha maonesho hayo maarufu kama ''Wiki ya Tanzania nchini Kenya'' ambayo yataenda sambamba na sherehe za miaka 54 za Muungano wa Tanzania.
|
Sehemu ya wadhamini na wajumbe wa kamati ya maandalizi wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiongozwa na Mhe. Waziri Mahiga (hayupo pichani) |
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.