Na Mwandishi wetu, Arusha
Baraza la Mawaziri la kisekta la Biashara, Viwanda,
Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki kujadili wanategemea kukutana kesho tarehe 28 Mei 2021 Jijini Arusha
kujadili masuala mbalimbali ya kukuza biashara na uwekezaji ndani ya Jumuiya
hiyo.
Mkutano huo wa Mawaziri umetanguliwa na mkutano wa Makatibu Wakuu wa sekta ya Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) wa Jumuiya hiyo uliofanyika leo jijini Arusha ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamepokea na kujadili ripoti mbalimbali ikiwemo ripoti za baraza la kisekta la mawaziri wa fedha, ripoti ya kamati ya forodha, ripoti ya kamati ya biashara, ripoti ya kamati ya viwango ya Afrika Mashariki, ripoti juu ya masuala ya ushindani pamoja na ripoti ya kamati ya uwekezaji.
Mkutano wa Makatibu Wakuu wa leo tarehe 27 Mei 2021 utafuatiwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa kisekta tarehe 28 Mei 2021 jijini Arusha.
Mwenyekiti wa
Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na
Uwekezaji (SCTIFI) ngazi ya Makatibu Wakuu, ambaye pia ni Katibu Mkuu, Wizara
ya Afrika Mashariki kutoka Kenya, Dkt. Kevit Desai akiongea na wajumbe wa
mkutano ulifanyanyika leo Jijini Arusha
Katibu Mkuu,
Wizara ya Viwanda na Biashara na Mkuu wa Ujumbe wa Tanzania, Bw. Doto James akifafanua
jambo katika mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sekta ya
biashara, viwanda, fedha na uwekezaji (SCTIFI) ulifanyanyika leo
Jijini Arusha. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Prof. Godius Kahyarara na kulia ni Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban.
Ujumbe wa Burundi ukifuatilia mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sekta ya biashara, viwanda, fedha na uwekezaji (SCTIFI) ulifanyanyika leo Jijini Arusha
Ujumbe wa Kenya
ukifuatilia mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sekta ya
biashara, viwanda, fedha na uwekezaji (SCTIFI) ulifanyanyika leo
Jijini Arusha
Baadhi ya wajumbe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
wakifuatilia mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sekta ya
biashara, viwanda, fedha na uwekezaji (SCTIFI) leo Jijini Arusha
Wajumbe
wakifuatilia mkutano
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.