Na Mwandishi wetu
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM), Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete ameongoza Kongamano la Maadhimisho
ya miaka 40 ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na kutoa uzoefu na
mchango wa Tanzania katika Jumuiya hiyo.
Rais
Kikwete amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa SADC ni kupunguza utegemezi, kukuza
ushirikiano utakaojenga mtangamano wa kikanda, kuhamasisha utekelezaji wa sera
za mipango ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za pamoja katika mpango wa maendeleo
na mpango wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama.
“Maadhimisho
haya yanaadhimishwa na nchi zote wanachama wa SADC kwa lengo la kutoa fursa ya kuangalia
na kutambua malengo, mchango na fursa zilizopo katika nchi wananchama wa SADC,“
amesema Dkt. Kikwete.
Dkt.
Kikwete ameongeza kuwa wapigania uhuru kutoka nchi nyingi za Afrika wanaendelea
kuikumbuka Tanzania kutokana na mchango mkubwa wa kuanzisha harakati za
kuzikomboa nchi nyingine kutoka katika utawala wa kikoloni ikiwa ni pamoja na
Tanzania kuwapatia mbinu za kupambana na Wakoloni.
Awali,
akiwasilisha salamu za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki kwa niaba ya Mhe. Waziri, Balozi Liberata Mulamula (Mb), Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine
amesema kuwa maadhimisho ya miaka 40 ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC) pamoja na masuala mengine, yanalenga kuenzi mchango mkubwa wa Viongozi
Wakuu waanzilishi wa SADC ambao maono yao yaliweka msingi wa ukombozi wa
kisiasa na kiuchumi kwa Kanda ya Kusini mwa Afrika; na Kuongeza uelewa wa
wananchi kuhusu mtangamano wa SADC na faida za uanachama wetu kwenye Jumuiya
hii ikiwa ni pamoja na fursa zilizopo katika nyanja mbalimbali ili waweze
kuzichangamkia.
“Tunapoadhimisha
miaka 40 ya SADC hatuwezi kamwe kuepuka kuzungumzia mchango mkubwa uliotolewa
na Tanzania kwenye Jumuiya hii.
Itakumbukukwa kuwa, Tanzania wakati wa uongozi wa Hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere ilifanya kazi kubwa ya kusaidia harakati za ukombozi hususan
kwa nchi za Kusini mwa Afrika. Kadhalika, Hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere alikuwa Mwenyekiti wa Kwanza wakati wa SADCC kabla ya kubadilishwa kuwa
SADC mwaka 1992,” amesema Balozi Sokoine.
Ameongeza
kuwa, Uenyekiti wa Tanzania katika SADC kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma,
ulikuwa wa mafanikio kwa nchi na kwa Kanda kwa ujumla. Miongoni mwa mafanikio
makubwa tunayojivunia ni kuridhiwa kwa Lugha yetu ya Taifa, Kiswahili kuwa
miongoni mwa Lugha nne za SADC.
“Ili
SADC itimize malengo iliyojiwekea ya kuwa Jumuiya yenye amani, usalama, ustawi
na maendeleo kama ilivyoelezwa kwenye Dira ya SADC ya mwaka 2050 na Mpango Mkakati wa Maendeleo wa Kanda 2020 -
2030 kila mdau lazima atimize wajibu wake umpasao,” amesema Balozi Sokoine.
Nae
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda amesema
kuwa nchi wanachama nyingine zinakiri na kutambua mchango wa Tanzania katika
harakati za kuzikomboa kutoka kwenye utawala wa kikoloni.
“Nchi
hizo zimekuwa zinakiri kuwa bila Tanzania kuzisaidia zingechelewa kupata uhuru
ikiwemo Afrika Kusini ambayo katika jitihada za kutafuta Uhuru wake ilimwaga
damu,” amesema Mhe. Makinda.
Pamoja
na hayo Mhe. Makinda amesema kuwa mchango wa Hayati Mwalimu Julius Nyeyere utaendelea
kukumbukwa daima na nchi wananchama wa SADC.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akiwasilisha mada kuu kwa
washiriki (hawapo pichani) katika Kongamano la Maadhimisho ya miaka 40 ya
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika: Uzoefu wa Tanzania
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph
Sokoine akiwasilisha salamu za Wizara kwa washiriki (hawapo pichani) katika
kongamano la maadhimisho ya miaka 40 ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Liberata Mulamula. Kongamano hilo limefanyika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akiwasilisha mada kuu kwa
washiriki wa Kongamano la Maadhimisho ya miaka 40 ya Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC): Uzoefu wa Tanzania
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda akichangia
mchango wa Tanzania katika historia ya SADC wakati wa Kongamano la Maadhimisho
ya Miaka 40 ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) lililofanyika
katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Kongamano
la miaka 40 ya SADC likiendelea
Washiriki
wakifuatilia Kongamano la miaka 40 ya SADC likiendelea
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.