Awali hoja ya kuivunja Tume ya Kiswahili ambayo ni moja ya Taasisi za Jumuiya iliwasilishwa kupitia ripoti ya mshauri mwelekezi na kuungwa mkono na takriban Nchi zote
Wanachama isipokuwa Tanzania kama moja ya mikakati ya kupunguza gharama za
uendeshaji ndani ya Jumuiya. Hata hivyo,nchi hizo ziliafiki kwa kauli moja hoja zilizolizotolewa na Tanzania kuhusu umuhimu wa Tume hiyo.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo ambaye pia ni Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba alieleza umuhimu wa Tume hiyo na kwamba ni kielelezo pekee muhimu cha Jumuiya na kuwataka kuunga mkono hoja ya kuiboresha na
kuiimarisha ili iendelee kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
“Hoja
ya kuvunja Tume ya Kiswahili kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji wa Jumuiya
inalenga kudidimiza malengo na misingi iliyopo ya kuiunganisha jumuiya. Hivyo nasisitiza
kuwa bado upo umuhimu mkubwa wa kuienzi Tume hiyo ambayo ni kielelezo muhimu cha
Jumuiya badala ya kufikiria kuivunja” alisema Mhe. Nchemba.
Awali, akifungua
mkutano huo, Mwenyekiti ambaye ni Waziri wa Fedha wa Kenya, Mhe. Ukur Yatani
Kanacho, alisema ana matarajio makubwa mkutano huo utafanyika kwa mafanikio na
kutoa pole kwa niaba ya Mawaziri walioshiriki Mkutano huo kwa Ujumbe wa
Tanzania na Serikali kwa ujumla kwa kuondokewa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati
Dkt. John Pombe Magufuli. Pia alitoa pole kwa Nchi Wanachama kufuatia janga la
ugonjwa wa Corona na kuwataka wajumbe kuendelea kushirikiana kwenye mapambano
dhidi ya ugonjwa huo.
Mkutano
huo pamoja na mambo mengine umepokea na kujadili agenda mbambali zilizowasilishwa
ikiwemo taarifa za Kamati zinazoshughulikia masuala ya Fedha ikiwemo ile ya
Makamishna Wakuu wa Mamlaka za Mapato za Nchi Wanachama pamoja na taarifa ya Utafiti wa kuboresha Mifumo na
Miundo ya Uendeshaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kulingana na rasilimali
zilizopo.
Ujumbe
wa Tanzania kwenye Mkutano huo umewahusisha pia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji
Uchumi na Ajira Zanzibar, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga, Waziri, Ofisi ya Rais,
Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango,
Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na
Uwekezaji, Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na
Mipango, Bi. Amina HK. Shaaban na Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini.
Mkutano huo ambao umeitishwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ulitanguliwa na kikao cha Ngazi ya Wataalam kutoka Sekta za Fedha na Uchumi uliofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Mei 2021 na kufuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika tarehe 6 Mei 2021.
Ujumbe wa Burundi ukiongozwa na Mhe. Balozi Ezechiel Nibigira (katikati) wakishiriki Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki |
Wajumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa kwenye Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki |
Mhe. Waziri Nchemba kwa pamoja na Mawaziri kutoka Zanzibar wakifuatilia Mkutano. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji, Uchumi na Ajira Zanzibar, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga |
Mhe. Balozi Nibigira kutoka Burundi akichangia jambo |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali na Kamishna Msaidizi, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. James Msina |
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki |
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania |
Ujumbe wa Tanzania |
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania |
Mkutano ukiendelea |
Wajumbe wakifuatilia mkutano |
Mkutano ukiendelea |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.