Na Mwandishi wetu, Mwanza
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeungana na Wizara, Taasisi,
Mashirika na Kampuni binafsi katika kushiriki maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza.
Maadhimisho
hayo yameongwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiambatana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim
Majaliwa Majaliwa (Mb), Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Husein Kattanga, Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb), Mawaziri wa
wizara mbalimbali pamoja na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama.
Watumishi
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameongozwa na
Waziri wake Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb), Naibu Waziri Mhe. Balozi Mbarouk
Nassoro Mbarouk (Mb) pamoja na Katibu Mkuu Mhe. Balozi Brigedia Jenerali
Wilbert Ibuge.
Kaulimbiu
katika maadhimisho hayo ni Maslahi bora, Mishahara juu, Kazi iendelee.
Watumishi
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika
maandamano ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza
Watumishi
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika
maandamano ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza meza kuu kushuhudia maandamano ya
Watumishi wa Umma na binafsi waliokuwa wakipita mbele ya jukwaa kuu wakati wa
kilele cha siku ya wafanyakazi duniani (hawapo pichani) iliyoadhimishwa kitaifa
katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula (Mb)
akiteta jambo na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb)
wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani iliyofanyika jijini Mwanza
katika uwanja wa CCM Kirumba
Sehemu
ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali wakifuatilia maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi Duniani iliyofanyika kitaifa jijini Mwanza
Sehemu
ya Mawaziri wa Wizara mbalimbali na Wakuu wa taasisi mbalimbali wakifuatilia maadhimisho
ya siku ya wafanyakazi Duniani iliyofanyika kitaifa jijini Mwanza
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.