Na Mwandishi wetu, Dar
Serikali imesema mwamko wa
biashara na uwekezaji ni mkubwa kwa sasa baada ya baadhi ya makampuni na
taasisi zilizokuwa zimefunga shughuli zao kuanza kurejea na kwamba serikali kwa
sasa inapitia upya sera yake ya uwekezaji ili kuweka mazingira bora Zaidi ya
biashara na uwekezaji.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameyasema hayo
alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe. Jeroen
Verheul Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa tamko la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kuhusu kuimarisha mazingira ya
uwekezaji na biashara yanakuwa rafiki.
“Mwamko wa biashara na
uwekezaji ni mkubwa kwa sasa baada ya baadhi ya makampuni na taasisi zilizokuwa
zimefunga shughuli zao kuanza kurejea na kwamba serikali kwa sasa inapitia upya
sera yake ya uwekezaji ili kuweka mazingira bora na salama zaidi ya biashara na
uwekezaji,” amesema Balozi Mulamula.
Balozi wa Uholanzi hapa Nchini
Mhe Jeroen Verheul amekiri kuwa Tanzania ina fursa na rasilimali nyingi
zinazohamasisha na kuvutia biashara na uwekezaji licha ya uwepo wa maeneo
machache yanayohitaji maboresho ambayo yakifanyiwa kazi ipasavyo makampuni
mengi kutoka Ulaya na mabara mengine yatakuja kuwekeza Nchini.
“Tanzania ina fursa na rasilimali
nyingi za uwekezaji licha ya uwepo wa maeneo machache yanayohitaji maboresho
ambayo yakifanyiwa kazi ipasavyo kampuni nyingi kutoka Ulaya na mabara mengine na
hata hapa Tanzania zitakuja kuwekeza kwa wingi,” amesema Balozi Verheul
Balozi huyo ameongeza kuwa
kupitia kauli mbiu ya diplomasia ya uchumi nchi yake iko tayari kushirikiana na
Tanzania katika kuangalia maeneo yenye changamoto na kuyatafutia ufumbuzi kwa
maslahi ya pande zote mbili.
Katika tukio jingine,
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma amekabidhi ofisi kwa Katibu Mkuu mpya Mhe. Joseph Edward Sokoine ambapo
tukio hilo limeshuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Liberata Mulamula.
Balozi wa Uholanzi hapa nchini
Mhe. Jeroen Verheul akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati walipokutana kwa mazungumzo
katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiteta jambo na
Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe. Jeroen Verheul wakati walipokutana kwa
mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo baina ya Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) na
Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe. Jeroen Verheul yakiendelea katika Ofisi
ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo baina ya Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) na
Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe. Jeroen Verheul yakiendelea katika Ofisi
ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika picha ya pamoja na Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe. Jeroen Verheul pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Hassan Mwamweta (mwenye tai nyekundu) na maafisa waandamizi kutoka wizarani pamoja na ubalozi wa Uholanzi
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.