Na Mwandishi wetu, Arusha
Timu ya wataalamu
kutoka Tanzania imekutana na timu ya wataalamu kutoka Kenya Jijini Arusha
kujadili njia za kuondoa vikwazo visivyo vya kibiasha baina ya Nchi hizo kwani
vimekuwa vikiathiri biashara, mkutano wa leo Mei 26, 2021 ni maandalizi ya
mkutano wa Mawaziri wa Biashara wa pande zote mbili utakaofanyika tarehe 29 Mei
2021.
Mkutano wa leo
utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 28 Mei 2021 na
baadaye mkutano wa Mawaziri tarehe 29
Mei 2021. Mkutano huo utahitimishwa kwa mawaziri wa Kenya na Tanzania kufanya
ziara katika mpaka wa Namanga tarehe 30 Mei, 2021 kujionea shughuli za biashara
zinavyofanyika katika mpaka huo.
Ujumbe wa Tanzania katika
timu wataalam umeongozwa na Mkurugenzi wa Mtangamano wa Biashara kutoka Wizara
ya Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu wakati ujumbe wa Kenya umeongozwa na Bw. Michael
Mandu, Mkuu wa Biashara baina ya Nchi na Nchi, Idara ya Maendeleo ya Biashara
na Ujasiriamali.
Mkutano wa wataalamu umetoa
fursa ya kujadili masuala yote yanayokwamisha biashara baina ya pande zote mbili
ambapo masuala yaliyowasilishwa na Kenya kujadiliwa ni pamoja na kutotoa upendeleo
kwa sigara, maziwa, bidhaa za nyama, kutoka Kenya, tozo ya kuingia kwa
wafanyabiashara (business pass) kufanya kazi za muda mfupi za kitaalamu.
kwa upande wa Kenya, baadhi
ya masuala ambayo Tanzania imewasilisha kujadiliwa ni kuongezwa bei ya vinywaji
baridi (uplifting) kutoka Tanzania, kutoza ushuru wa forodha bidhaa za glass,
kuzuia mahindi kutoka Tanzania, bei kubwa ya ushuru wa stempu katika bia,
kubadili mfumo wa uingizaji mizigo mikubwa ambapo gharama za uingizaji mizigo Kenya
zimeongezeka na kuathiri biashara.
Katika kutekeleza
maagizo ya Wakuu wa nchi (Tanzania na Kenya) mawaziri wa seka husika kutoka watakutana
na kujadili juu ya vikwazo hivyo katika mkutano wao utakaofanyika tarehe 29
Mei, 2021 jijini Arusha.
Tarehe 4 – 5 Mei, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alifanya
ziara rasmi nchini Kenya ambapo katika ziara hiyo Mhe. Samia Hassan Suluhu na
Mwenyeji wake Mhe. Uhuru Kenyatta pamoja na mambo mengine, walielekeza Mawaziri
wa Biashara wa pande zote wakutane na kujadili vikwazo vya kibiashara ambavyo
vinaathiri biashara kwa lengo la kuviondoa.
Mwenyekiti wa timu ya
majadiliano ambae ni Mkurugenzi wa Mtangamano wa Biashara kutoka Wizara ya
Viwanda na Biashara – Tanzania, Bw. Ally Gugu akiongea na washiriki (hawapo
pichani) wakati wataalamu hao walipokutana leo Jijini Arusha kujadili njia za
kuondoa vikwazo visivyo vya kibiasha baina ya Tanzania na Kenya. Kulia ni mwenyekiti
mwenza kutoka Kenya ambae ni Mkuu Kitengo cha Biashara baina ya Nchi na Nchi,
Idara ya Biashara na Maendeleo ya Ujasiriamali Bw. Michael Mandu.
Sehemu ya ujumbe wa
Tanzania ukifutilia mkutano wa madajiliano ya kuondoa vikwazo visivyo vya
kiforodha
Sehemu ya ujumbe wa
Tanzania ukifutilia mkutano wa madajiliano ya kuondoa vikwazo visivyo vya
kiforodha
Timu ya wataalam kutoka
Tanzania na Kenya wakifuatilia mkutano wa madajiliano ya kuondoa vikwazo
visivyo vya kiforodha
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.