=============================
Before
I start my speech, let me also recognize the presence of Honorable Minister
Stephen Wasira the Seventh Day Adventist disciple, who
has traveled 500 kilometers to be here. Mheshimiwa Wasira karibu
sana.
Before
I continue with my speech let me also mention other government officials who
are also members of the SDA apart from Honorable Wasira;
The
Chief Secretary, Hon. Sefue is an SDA member,
The
Attorney General of Tanzania Mr. Masaju is an SDA member,
The
Permanent Secretary Mr. Maswi of Energy and Mineral, is an SDA member,
So,
I mean there are so many others in government that are not only members but
they acknowledge many good things that the SDA has been doing.
….continue
in English version, see the Swahili translation….
Before I start my speech, let me also recognize the presence of Honorable Minister Stephen Wasira the Seventh Day Adventist disciple, who has traveled 500 kilometers to be here. Mheshimiwa Wasira karibu sana.
Before I continue with my speech let me also mention other government officials who are also members of the SDA apart from Honorable Wasira;
The Chief Secretary, Hon. Sefue is an SDA member,
The Attorney General of Tanzania Mr. Masaju is an SDA member,
The Permanent Secretary Mr. Maswi of Energy and Mineral, is an SDA member,
So, I mean there are so many others in government that are not only members but they acknowledge many good things that the SDA has been doing.
….continue in English version, see the Swahili translation….
Kwa muhtasari tu kwa
Watanzania mlioko wengi, na Watanzania wanaotusikiliza;
Nimemshukuru Rais wa
Baraza Kuu la Makanisa ya Sabato Duniani, kwa kujumuika nasi na kuamua Tanzania
kuwa mwenyeji wa Kongamano hili kubwa sana la bara la Afrika.
Na ni imani yangu
kwamba mtapokea salamu hizi nilizotoa kwa niaba ya Serikali…...
Nimemshukuru kwa
mwaliko wake kwangu kuja kujumuika nanyi na kufunga Kongamano hili. Nimekubali
kwa sababu mbili, kwanza, jambo lenyewe hili la kiroho mnalosimamia na
kulifanya ni jambo jema sana kwa ustawi wetu sote. Pili, kongamano hili ni la
kimataifa na hivyo linauhusiano na kazi yangu ya uanadiplomasia. Katika miaka 9
ya kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na miaka 8 ya kuwa Mshauri wa Balozi wa Tanzania
nchini Canada, nimejifunza kuwa diplomasia na hofu ya Mungu/imani vikifanya
kazi kwa kushirikiana, hakuna changamoto yoyote ya kidunia isiyoweza
kukabiliwa. (MAKOFI)
Nimezungumzia
uhusiano kati ya Serikali na Dini. Nimesema kuwa vitu hivi viwili
havitenganishiki, ni sura mbili za sarafu. Kwa sababu, binadamu ni mwili na
roho na kila kimoja hakina budi kuendelezwa. Serikali inashughulika na miili na
akili, Dini zinashughulika na roho. Dini na Serikali zikifanya kazi pamoja
sawasawa, tutahitaji sheria chache, polisi wachache, magereza machache. Dunia
itakuwa mahala pazuri pa kuishi. Tunahitajiana.(MAKOFI)
Wenzetu wa vyombo vya
dini wanahubiri amani wanakiri imani, sisi wanadiplomasia na Serikali
tunatengeneza amani na wakati mwingine tunatumia vyombo vya dola kuitengeneza
hiyo amani. Kwa hiyo lengo letu ni moja, kuleta amani, utulivu, katika nchi.
Wenzetu njia yao ni nyembamba --sorry-- ni nyembamba lakini ina mapana na ni nzuri zaidi, kuliko ile
tunayoitumia sisi. (MAKOFI)
Lakini diplomasia na dini zinakutana kwenye kukuza amani,
ulinzi na usalama duniani.
Lakini pia tunakutana
kwenye maadili. Viongozi wanaolelewa vizuri na dini zao, wanakuwa waadilifu. Na
SDA ni miongoni mwa dini zinazoweka viongozi wazuri sana wa nchi yetu. (MAKOFI)
Na kwasababu hiyo
basi, unapoona diplomasia inatengeneza mahusiano mazuri ya dunia, dunia inaangalia
uadilifu kwanza, kama kigezo cha uongozi bora, na kama kigezo cha watu wenye
amani na utulivu. Na kawaida Serikali, diplomasia na dini hata Rais mwenyewe, tunakutana
tunapozungumzia masuala ya uadilifu wa viongozi wake. (MAKOFI)
Tunzeni hiyo,
hubirini uadilifu, na mshiriki katika kutengeneza viongozi bora kwa misingi ya
uadilifu. (MAKOFI)
Lakini jingine, nimeshukuru
sana Kanisa la Sabato kwa kazi na mwenendo mzuri unaofanywa katika nchi yetu. Unapoona
kwamba watu milioni nne waliomo nchini kwetu, wa SDA, wana shule za msingi 10, wana
shule za sekondari 15, wana vyuo vikuu 2, wana hospitali kubwa 2, wana vituo
vya albino vinavyofanya kazi hapa nchini. (MAKOFI)
Hivi kama kingekua chama cha siasa,
nani angeshindwa kuwapa ushindi wa utawala wa nchi hii. (MAKOFI)
Nani angeshindwa
kuwapa ushindi. Lakini ukiachia hayo, ni Chama cha Mapinduzi peke yake chenye
kumudu kazi hiyo. (MAKOFI, VIGELEGELE, VICHEKO)
Lakini naomba niweke
wazi kabisa, kama chombo cha dini, kama SDA, kinajali wananchi wake, kitaacha
vipi kupanuka kutoka watu 15,000 mwaka 1960 hadi kufikia watu milioni nne mwaka
2012. (MAKOFI) Wataacha vipi kupanuka na kuwa watu wengi kwa huduma hii,
wanayoitoa kwa wananchi. (MAKOFI)
Nawapongeza sana watu
wa SDA, mbele ya kiongozi wenu wa dunia, kwa kazi nzuri mnayoifanya na shule
mnayofundisha Watanzania kwamba ukitaka kuongoza Watanzania, fanya kama SDA. (MAKOFI)
Nalipongeza kanisa la
SDA kuwa mfano mzuri wa ustahimilivu na uvumilivu wa dini na imani katika
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika miaka yangu yote ya nafasi yangu ya
uwaziri, na kaka yangu Mzee Wasira ataniunga mkono kwenye hili, sijawahi
kusikia mgogoro wa kimatatizo wala mfarakano unaoongozwa na SDA (MAKOFI) dhidi
ya madhehebu mengine, au dhidi ya wananchi. (MAKOFI)
Mpo, mnafanya kazi
zenu, mnachapa shuguli zenu kwa amani na utulivu, hamjachokoza mtu, na
hamtachokoza mtu, na hiyo ni sifa mojawapo ya nchi yenye amani duniani.
(MAKOFI)
Hongereni sana wana
SDA. (MAKOFI)
Narudia, kama
wananchi wote wa dini zote tukiiga mfano wenu, Tanzania tutasonga mbele kama
Taifa. (MAKOFI)
Nawashukuruni kwa
kunisikiliza na ninawatakia maandalizi mazuri ya kongamano la kidunia
litakalofanyika baadae mwaka huu huko Marekani. (MAKOFI)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.