Wednesday, February 18, 2015

Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Mabalozi kutoka Malawi, Kuwait, Afrika Kusini na Kenya


...Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Malawi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambuliosho kutoka kwa Balozi mpya wa Malawi hapa nchini, Mhe. Hawa Olga Ndilowe. Balozi Ndilowe amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Marehemu Balozi Flossie Gomile-Chidyaonga aliyefariki ghafla mwezi Mei 2014. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 18 Februari, 2015
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Ndilowe mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha  na Balozi Ndilowe pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)  (mwenya tai ya bluu) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Mhe. Prof. Mark Mwandosya (wa kwanza kulia) pamoja na baadhi ya Maafisa kutoka Ubalozi wa Malawi hapa nchini.
Balozi Ndilowe akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu kabla ya kukabidhi Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Kikwete
Balozi Ndilowe akisikiliza wimbo wa taifa lake uliopigwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kukabidhi Hati za Utambulisho. Kulia ni Balozi Mohamed Maharage Juma , Mkuu wa Itifaki na Kaimu Mnikulu, Bw. Fyataga
Brass Band ya Polisi wakipiga wimbo wa taifa wa Malawi kwa heshima ya Balozi Ndilowe.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana wakati wa mapokezi ya Balozi mpya wa Malawi hapa nchini Mhe. Ndilowe.
Maafisa kutoka Ubalozi wa Malawi hapa nchini wakiwa na Bi. Mercy Kitonga, Afisa Mambo ya Nje wakifutilia taratibu za mapokezi ya Balozi Ndilowe (hayupo pichani)
Balozi Ndilowe akiagana na Kiongozi wa Bendi ya Polisi mara baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho kwa Balozi.

...Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Kuwait

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambuliosho kutoka kwa Balozi mpya wa Kuwait  hapa nchini, Mhe. Jasem Ibrahim Al-Najem. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 18 Februari, 2015.
Balozi Al-Najem akisalimiana na Waziri Membe mara baada ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. Rais Kikwete
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi Al-Najem
Mhe. Rais Kikwete na Balozi Al-Najem katika picha ya pamoja na Waziri Membe, Prof. Mwandosya na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya (kulia)
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi Al-Najem
Balozi Al-Najem akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ikulu
Balozi Al-Najem akisikiliza wimbo wa taifa lake wakati wa mapokezi yake Ikulu.
Bendi ya Polisi ikipiga wimbo wa Taifa wa Kuwait na Tanzania


...Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Afrika Kusini



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambuliosho kutoka kwa Balozi mpya wa Afrika Kusini hapa nchini, Mhe. Thamsanqa Dennis Mseleku. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 18 Februari, 2015.
Balozi Mseleku akisalimiana na Waziri Membe
Balozi Mseleku akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Balozi Yahya huku Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundala akishuhudia


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (kulia) pamoja na Bi. Talha Mohamed na Bw. Mudrick Soragha wakifuatilia kwa makini tukio la uwasilishaji Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Afrika Kusini hapa nchini (hayupo pichani)


Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Balozi Mseleku mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu (kulia) akiwa na Mshauri wa Rais masuala ya Diplomasia, Balozi Samwel Shelukindo (kushoto) na Bi. Bundala wakinukuu mazungumzo kati ya Mhe. Rais na Balozi Mseleku (hawapo pichani)

...Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Kenya


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambuliosho kutoka kwa Balozi mpya wa Kenya hapa nchini, Mhe. Chirau Ali Mwakwere. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 18 Februari, 2015.
Mhe. Rais Kikwete akiwa kwenye mazungumzo na Balozi Mwakwere
Picha ya pamoja






No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.